Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Afia Gesti akiwa na mke wa mtu

$
0
0

castle-lodge-guest-house

Kumradhi picha hii haihusiani na tukio hili. (Picha kwa msaada wa Mtandao)

.Marehemu alikuwa anatembea na mke wa rafiki yake kitambo 

Na Mwandishi Wetu, MOblog

Katika hali isiyokuwa kawaida Mtu mmoja kwa sasa (Jina Linahifadhiwa) amekutwa amekufa kwenye nyumba ya wageni (Lounge) maeneo ya Mbezi Kimara nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mashuhuda wanasema kwamba marehemu (Jina linahifadhiwa kwa sasa) alikuwa anatembea na mke wa mtu ambaye ni jirani yake maeneo ya magari saba na ni marafiki wa karibu.

Habari zilizotufikia tangu jana usiku ni kwamba Baba huyo ambaye (jina tunalo) ambaye yeye na huyo mke wa mtu wanakaa maeneo ya magari saba na  ni (Family Friend) kwa kitambo kidogo alikuwa na mazoea ya kutembea na mke wa rafiki yake.

Mpaka tunakwenda hewani mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Tumbi Kibaha baada ya marehemu kufariki ndani ya Lounge hiyo baada ya kumeza vidonge vya kuongeza nguvu.

r-SENIOR-SEX-large570

“Huyo Baba naniii alikuwa na tabia ya kutembea na mke wa jirani yake kwa hiyo siku ya tukio yaani juzi usiku alikunywa vidonge vya kuongeza nguvu na pombe ili akafanye uzinzi na mke wa rafiki yake kwa bahati mbaya hali ikabadilika ghafla na mama huyo kukimbia,” amesema mmoja wa washuhuda maeneo ya Mbezi Inn

Amesema Marehemu alikuwa na tabia ambayo hata majirani zake wamepigwa na butwaa baada ya habari hizo kuzagaa katika mitaa ya kadhaa maeneo ya Kibamba, Mbezi Inn, Kwa Yusufu na Kimara kuhusu kifo chake.

Mtoa taarifa anasema Polisi walifanikiwa kumkamata mama huyo baada ya kuangalia simu ya marehemu na kuona mtu wa mwisho kuwasiliana naye na kumpiga kisha kumdaganya kwamba mwenzake yupo tumbi na anaendelea vizuri.

Mtoa taarifa anasema baada ya kufika Tumbi akakutana na mkono wa dola na mpaka sasa yupo ndani na upelelezi unaendelea wa tukio hilo la kusikitisha.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles