Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 akiwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIVYAWATA) Bw. Amon Anastaz akisoma risala kwa kutumia braille katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipongeza baada ya kupokea risala toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (SHIRYAWATA) akisoma risala kwa kutumia Braille huku mkalimani wa lugha ya alama akifanya kazi hiyo (kulia) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013 kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua rasmi alama mpya za barabarani kwa watu wenye ulemavu wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Usalama barabarani ya Watu wenye Ulemavu (NCPDRS) na mbunifu wa alama za barabarani kwa watu wenye ulemavu ,Bw. Jutoram Kabatelle,kabla ya kuzindua rasmi alama mpya kwa watu wenye ulemavu wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Bi. Lupi Maswanya kwa kutumia akitoa shukrani kwa lugha ya alama huku mfasili akitafsiri kwa sauti wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikweteakipokea tuzo toka kwa Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu, Bi. Lupi Maswanya wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo Novemba 3, 2013
Picha juu na chini ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitembelea mabanda ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na watu wenye ulemavu wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wadau wa SHIVIWATA wakati wa sherehe ya Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam leo.(Picha na IKULU).