Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

“Nina cement Kali ya Kuziba Mpasuko TPA”– Dr Mwakyembe

$
0
0

mbe 2

Na. Mwandishi wetu.

Waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe (pichani) ameipa siku moja Menejimenti ya Mamlaka ya Bandari (TPA) kutaja majina ya watu wanaoiba mafuta katika bomba kubwa la kupakulia mafuta bandarini (SBM) au vingine waonje joto la Segerea. Pia ameomba picha za walinzi mabomba haya ili ziweze kutolewa kwenye magazeti kwamba wanashirikiana na wezi hao bila kuwakata.

Alisema wezi hao bila woga wowote wametoboa bomba hilo ambalo ujenzi wake umeigharimu serikali Billioni 60 ya fedha za mkopo, kuunganisha mabomba yao chini kwa chini ndani ya maji kisha kunyonya mafuta hadi kwenye vituo vyao vya kuhifadhia mafuta,………Alisema wezi hao wamekuwa wakiibia serikali lita 135,000 hadi 140,000 za mafuta kwa siku. Ujenzi wa bomba hilo ulikamilika takriban mwaka mmoja uliopita.

“Haiwezekani wizi huo ukafanyika bila TPA kuwajua wahusika kwa sababu hujuma hii inaonyesha kuwa inafanywa na watu wenye utaalamu wa hali ya juu tena wanaojuwa kupiga mbizi na kukaa ndani ya maji kwa muda mrefu kiasi cha kutuboa bomba, kuunganisha hadi kwenye matanki yao,” alisema Dk Mwakyembe wakati akizungumza na wafanyakazi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam kuhusu changamoto na mafaniko katika utendaji wao wa kazi, nawahakikishieni nina simenti special ya kuziba mipasuko na mianya yote ya mipasuko, naomba wananchi tushirikiane kwa pamoja.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles