Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Kitabu cha Miaka 10 ya Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika(SADCOPAC) baada ya Kufungua Mkutano wa mwaka wa WA SADCOPAC kwenye kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC Septemba 2, 2013. Kulia kwake ni Spika wa Bunge Anne Makinda.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisindikizwa na Spika wa Bunge, Anne Mkinda (kulia) na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Ludovic Utouh baada ya kufungua Mkutano wa Mwaka wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCOPAC) kwenye kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC Septemba 2, 2013.
Mzee wa Kimasai akipuliza zumari wakati kikundi cha ngoma cha wamasai cha Arusha kilipotumbuiza katika mkutano wa mwaka wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCOPAC) kwenye kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC Septemba 2, 2013.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na washiriki wa Mkutano wa Mwaka wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kwa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADCOPAC) baada ya kufungua mkutano wao kwenye kituo cha Mikutano cha kimataifa cha Arusha AICC Septemba 2, 2013.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).