Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

SMZ na Kampuni ya Royal Dutch Shell zatiliana saini makubaliano ya uwekezaji wa sekta ya Mafuta na Gesi

$
0
0

Zanzibar

  Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Ramadhani Abdalla Shaaban akibadilishana Waraka wa  makubaliano na Mwenyekiti wa Shell Deepwater Tanzania Bw. Axel Knospe.

Na.Mwandishi wetu

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Kampuni ya Royal Dutch Shell plc (Shell) kwa pamoja wametangaza uwekaji saini wa Waraka wa Makubaliano.

Waraka huo unaweka bayana ushirikiano kati ya Kampuni ya Shell na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sekta ya Mafuta na Gesi na inafafanua hususan kuhusu hatua za awali zinazohusiana na kujenga uwezo katika sekta ya Mafuta na Gesi pamoja na Maendeleo ya Vijana katika kukuza ujuzi wao kwenye sekta hii, ikiwa ni pamoja na jitihada za elimu na uwezo wa ujasiriamali.

Axel Knospe, Mwenyekiti wa Shell Deepwater Tanzania alieleza kuwa, “Kampuni ya Shell ina nia ya kuwa na uhusiano imara na Serikali ya Zanzibar na pale itakapofaa, itaanza hatua za utafiti ambao utafanyika kwa njia endelevu, ya kiuchumi, kijamii na inayowajibika kimazingira”.

Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mh. Ramadhani Abdalla Shaaban alisema kuwa utiaji saini wa waraka huo ni hatua kubwa inayoonyesha jitihada za Serikali za kuendeleza sekta ya nishati Zanzibar.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles