Timu ya Bayern Munich ya Ujerumani imefanikiwa kutwaa ubingwa wa kombe la UEFA Super Cup baada ya kuitandika Chelsea ya Uingereza kwa mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penati, baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika muda wa nyongeza.
Penati zote tisa ziliutikisa wavu kabla mkwaju wa penati wa mchezaji wa Chelsea Romeu Lukaku, kuokolewa na golikipa wa Bayern Munich Manuel Neuer na kuwapa ushindi mabingwa wa Ulaya Bayern Munich dhidi ya mabingwa wa ligi ya Ulaya Chelsea.
Mechi hiyo ngumu ilichezwa katika uwanja wa Eden Arena mjini Prague katika Jamhuri ya Czech.
Chelsea ililazimika kucheza na wachezaji kumi baada ya Ramiress kupewa kadi ya pili ya njano katika dakika ya 85.
Kocha wa Bayern Pep Guardiola ameelezea furaha yake kutokana na mchezo ulioonyeshwa na wachezaji wake na kuibuka na ushindi, wakati kocha wa Chelsea Jose Mourinho amelalamika kuwa ana bahati mbaya.