Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mzee Nelson Mandela arejea nyumbani kutoka hospitali alikokuwa amelazwa.

$
0
0

MANDELA DISCHARGED

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela amerejea nyumbani kwake mjini Johannesburg kimya kimya baada ya kulazwa hospitali mjini Pretoria kwa muda mrefu.

Mandela mwenye umri wa miaka 95 alilazwa hospitali tangu Juni 8 mwaka huu baada ya kupata maambukizi katika mapafu.

Hali ya afya yake wiki iliyopita ilitajwa kuwa ‘mbaya lakini imara’ na haikutolewa taarifa tena kuhusiana na afya yake.

Maambukizi ya ugonjwa wake yanasemekana kuhusishwa na kipindi cha karibu miongo mitatu aliyokaa gerezani baada ya kufungwa kutokana na harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles