Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Ukuaji wa pato la taifa waongezeka kwa asilimia 7.5 kwa robo ya kwanza ya mwaka 2013.

$
0
0

DSC_0290

Mkurugenzi Takwimu za Uchumi Morrice Oyuke.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Wizara ya Fedha ina jukumu la kukokotoa pato la taifa kwa robo mwaka ili kuwapatia takwimu kwa wakati, wadau wa takwimu za pato la taifa katika vipindi vifupi vya robo mwaka ili kuweza kutathmini mabadiliko ya ukuaji wa uchumi.

Ukuaji halisi wa pato la taifa la Tanzania kwa bei za soko uliongezeka kwa kasi ya asilimia 7.5 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2013 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 7.4 katika kipindi kama hicho mwaka 2012.

Shughuli za kiuchumi za kilimo zilifikia kasi ya ukuaji ya asilimia 1.4 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2013 zikilinganishwa na asilimia 0.4 ya robo kama hiyo mwaka 2012.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Takwimu za Uchumi Morrice Oyuke amesema shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto zilishuka kwa kasi ya asilimia 4.7 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2013 ikilinganishwa na kasi ya ukuaji wa asilimia 23.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2012.

Amesema shughuli za biashara za jumla na reja reja, ukarabati wa magari na pikipiki na vifaa vingine vya majumbani zilifikia kasi ya ukuaji wa asilimia 9.5 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2013 ikilinganishwa na kasi ya asilimia 12.1 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2012.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Latest Images

Trending Articles



Latest Images