Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

AMREF yaandaa chakula cha hisani kuchangisha fedha za kampeni ya “Stand Up for African Mothers”

$
0
0

pic-23

 

Mkurugenzi wa Taasisi ya AMREF Tanzania Dk.Festus Ilako akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu  halfa ya chakula cha hisani ya kuchangisha fedha yenye kauli mbiu ya “Stand for African(Tanzania) Mother’s” ili kuchangia mfuko wa kuwasaidia wakina mama na watoto,halfa hiyo itafanyika Oktoba 11 mwaka huu katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Bi.Teddy Mapunda  na kulia ni Naibu Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dk, Rita Noronha.

Taasisi ya AMREF Tanzania imetangaza kuwa inatayarisha chakula cha hisani kuchangisha fedha kwa ajili ya kuchangia mfuko wa kuwasaidia akina mama na watoto itakayokuwa na kauli mbiu “Stand for African mothers“ ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. J akaya Kikwete.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa AMREF Tanzania Dkt. Festus Ilako alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Dkt. Ilako amesema kuwa hafla hiyo itafanyika Oktoba 11, 2013 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam ambapo taasisi yake inashirikiana na Serikali ya Tanzania katika kufanikisha malengo ya maendeleo ya Milenia ya kuboresha huduma za afya hasa za akina mama na watoto.

 Dkt. Ilako amesema “ili kufikia malengo hayo, kunahitajika kuwa na wakunga wa kutosha kuimarsha Nyanja ya uzazi salama kufanikisha malengo ya millennia”.

Tangu kampeni hiyo ianzishwe tayari wakunga 10 wamewezeshwa kupata elimu na wengine 70 wanategemewa kujiunga.

Ili kufanikisha malengo kuboresha huduma ya mama na mtoto kunahitajika uboreshaji wa ujuzi wa wakunga 2,800 kwa kutumia teknolojia ya kisasa ya “e-lerning “na kutoa mafunzoya awali kwa walau wakunga 1000 mpaka mwaka 2015.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Montage Tanzania Teddy Mapunda amesema kuwa wanaotarajiwa kuhudhuria ni pamoja na viongozi wakuu wa taasisi mbalimbali  za kiserikali, za binafsi ndani na nje ya nchi na wananchi wote

Mapunda pia amewaomba vyombo vya habari kuwa mabalozi wazuri ili watanzania wajue AMREF inafanya nini ili watanzania waweze kuwa na uzazi salama.

Kufanikisha azma hiyo Mapunda amewaomba watu wote wenye mapenzi mema kutoa  michango yao na kuiwasilisha kupitia huduma ya M-pesa kwa namba 0752-167286, au akaunti ya NBC makao makuu, 0111030004548 ama kununua meza ya watu kumi katika hafla hiyo  kwa kiasi cha dola 1500 sawa na shilingi 2,430,000 za kitanzania.   

Kampeni ya “Stand up for African Mothers” ilizinduliwa mwaka 2012 ambapo  AMREF ina zaidi ya miaka 57 katika kutoa huduma za kijamii sehemu mbalimbali.

Wadhamini wa hafla ya kuchangisha fedha hiyo ni benki ya AMREF ikishirikiana na benki ya NBC, Serengeti  Breweries  na ITV.

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles