Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Pinda afungua maonyesho ya elimu Dodoma

$
0
0

PG4A2164

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Sista  Flosy Sequeire, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Saint Francis ya Mbeya tuzo maalum ya kutambua  ufalu mzuri wa wanafunzi wa shule  hiyo  wakati alipofungua  maadhimisho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 2015. Wemgne kutoka kushoto ni  Waziri wa Elimu na Mafunzi ya Ufundi, Dkt. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Seriklai za Mitaa, Kassim Majaliwa, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa na Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PG4A2337
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi pikipiki Mratibu wa Elimu wa Kata ya Ibiwhwa wilayani Bahi, Jacob Mwakalambo ikiwa ni chombo cha kumwezesha kutekeleza majukumu yake katika maadhimisho ya wiki ya elimu wenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 15, 2015.  Kulia ni Naibu waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Kassim Majaliwa.
PG4A2343
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mzee wa Kihadzabe, Mandona katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 1015. Kulia ni Bibi Agnes Israel.
PG4A2420
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipata maelezo kuhusu shughuli mbalimbali za British Council wakati alipotembelea banda  la Taasisi hiyo kwenye maonyesho ya Elimu aliyoyafungua kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei  11, 2015.
PG4A2445
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizazama madawati ya gharama nafuu  wakati alipotembelea  Edosama Hardware watengenezaji wa madawati ya gharama nafuu baada ya kufungua wiki ya elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 2015. Kuliani  Oscar Kaduma na wapili kulia ni Edward Maduhu wote wakiwa ni watendaji wa kampuni hiyo. Kushoto ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, KassimMajaliwa.
PG4A2390
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimsikiza mtoto wa kabila la Wahadzabe,, Kone Paschal wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya bweni ya Mngulu mkoani Singida katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma Mei 11, 2015/(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles