Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

ACT Wazalendo wachangia damu hospitali ya Taifa Muhimbili

$
0
0

9

Muuguzi Mwandamizi Judith Kayombo akichanganya  Damu wakati alipokuwa akimtoa Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba.

Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba akisalimiana na Katibu wa Vijana Jimbo la Ukonga wakati wa uchangiaji Damu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na ikiwa  Chama hicho kikitimiza  Mwaka Mmoja toka kuanzishwa kwa chama hicho (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA).

 Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba akisalimiana na viongozi  mbalimbali  wa chama hicho kulia ni Afisa Habari wa chama hicho.

Mwenyekiti Ngome Wanawake Jimbo la Kinondoni Asma Miraji akimkabidhi kadi Omar Hashimu kujiunga na chama cha ACT mara walipofika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam , ambapo Dereva huyo alikua amemfata mkewe hospitalini hapo.

Mwenyekiti Ngome Wanawake Jimbo la Kinondoni Asma Miraji (kushoto) akimkabidhi kadi  Amina Kibwana (kulia) baada ya kuomba   kujiunga na chama cha ACT wakati wa  chamahicho lilipofika  katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salaam kuchangia Damu  katikati ni mfanyakazi wa Hospitali ya Taifa muhimbili Salama Kasembe

Wanachama wakimsikiliza kwa makini  Mnasihi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Ishengoma (pichani hayupo) alipokua akitowa maelezo kwa Wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo walipo fika Hospitalini hapo kuchangia Damu wakiongozwa na Katibu Mkuu Taifa wa Chama  hicho  cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba (kulia)

Wanachama wa chama cha ACT Wazalendo wakisubiri huduma huku Amir Kabwe (wakwanza kushoto) akimuelekeza jambo  Mwenyekiti Ngome Wanawake Jimbo la Kinondoni Asma Miraji (kulia).

Mnasihi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Ishengo akitowa maelezo kwa Wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo walipofika Hospitalini Hapo kuchangia Damu ikiwa  Chama hicho  kimetimiza Mwaka Mmoja toka kuanzishwa kwa Chama hicho.

 

Mkurugenzi Huduma za Tiba Shirikishi Daktari, Praxeda Ogweyo (wakwanza kulia)  akiwakaribisha na kuwashukuru wanachama wa Chama cha ACT Wazalendo kwaniaba ya Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  ambapo wanachama hao waliongozwa  na  Katibu Mkuu Taifa wa Chama   cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba  na anae mfatia kulia kwa Daktari  ni Mkurugenzi wa Idarara Maabara Kuu Hospitalini  hapo Daktar Alex Magesa.

Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba akishukuru kwa uongozi na mapokezi waliyoyapata Hospitalini hapo mara walipofika katika Hoapitali ya Taifa kuchangia Damu

Mwenyekiti Mkoa Hamis Chambuso akiiongea na waandindishi wa Habari (pichani hapo) akiomba watu kujitokeza.

Katibu Mkuu Taifa wa Chama  cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba akiweka Saini wakati alipokua akijianda kutolewa Damu kwa kuchangia kwa hiyari  alipofia Hospitalini hapo na wanachama Mbalimbali huku chama hicho kikitimiza Mwaka mmoja.

Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba (kushoto)  Amir Kabwe wakiwa wamelala katika vitanda Maalum kwa wachangiaji Damu.

Muuguzi Mkunga wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Ruth Geay (kushoto)  akimtoa Damu Amir Kabwe.

Muuguzi Mwandamizi Judith Kayombo akimtoa Damu Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba

Muuguzi Mwangamizi Judith Kayombo akiichanganya  Damu wakati alipokuwa akimtoa  Katibu Mkuu Taifa wa Chama cha ACT Wazalendo Samsoni Mwigamba.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles