Mwandishi Mwandamizi wa Modewji blog (mtandao huu), Andrew Chale akiwa ndani ya kituo cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani cha Ubungo, Jijini Dar es Salaam akiendelea ‘kusaka’ habari hasa kujionea mazingira ya abiria waliokuwa na watotom wagonjwa na wasiojiweza wanavyopata taabu usiku huu baada ya mgomo huo huku abiria wakilala kwenye magari waliokatia tiketi
Na Andrew Chale, Modewji blog
Hadi muda huu wa saa tano na nusu usiku (11:34 pm) leo Mei 4, Mtandao wako bora nchini wa Modewji Blog bado upo hapa stendi kuu ya mabasi yaendayo Mikoa mbalimbali na nchi jirani, Ubungo, tukiendelea kukupatia kile kilicho bora na kukuripotia kwa uhakika.
Kwa ujumla hali ni mbaya kwani wengi wa abiria waliopo hapa imewabidi kulala ndani ya mabasi hayo ambayo tayari wameshakatia tiketi huku wengine wakiamua kulala katika jengo maalum la kupumzikia wasafiri wanaosubiria mabasi kwa safari jengo ambalo lipo kaskazini mwa stendi hiyo ya mabasi.
Modewji blog, imeshuhudia watu mbalimbali ambao ni wasafiri wakiwa na mabegi yao wakichangamkia kununua mikeka iliyokuwa ikiuzwa ndani ya kituo hicho cha mabasi na kutandika kwa ajili ya kulalia. Kwa ujumla wasafiri hao, wapo katika hali mbaya, kwani wengi hawana mashuka ya kujifunika kujikinga na baridi.
Pia kwa walioamua kuingia kulala kwenye magari nao wakipata taabu kubwa kwani baadhi ya mabasi hayo viti vyao si rafiki kwa kuwawezesha katika matumizi hayo ya kulala humo zaidi ya kukaa.
Modewji blog kazini ‘Tunakuangazia ‘LIVE’ kutoka Ugungo
Hali ya Usalama!
Dulu za kihabari ambazo mtandao huu imezipata zinaeleza kuwa ndani ya kituo hicho majira ya usiku ni mbaya kwani vijana wa kihuni utumia mwanya huo kuibia abiria ikiwemo mizigo na kupora. Mmoja wa watu ambaye anafanya shughuli zake ndani humo, alibainisha kuwa, kuna kundi la vibaka ambao kazi yao kubwa ni kuibia abiria ama mali zao hasa nyakati za usiku kutokana na kutokuwa mazingira salama hasa karibu maeneo mengi kuwa na giza nene.
Modewji blog, ambayo ‘inarandaranda’ ndani ya kituo hichi imeshuhudia mazingira hayo magumu kwani karibu maeneo mengi yapo na giza totoro huku usalama ukiwa mdogo.
Waziri Mkuu aunda tume ya watu 13!
Hata hivyo, kufuatia, viongozi wa madereva hao kutoa tamko la kutoenda Ikulu kuonana na Waziri Mkuu kama walivyoombwa , Kwa upande wake, Waziri Mkuu ameunda tume ya watu 13, kushughulikia tatizo la mmadereva nchini. Kwa mujibu wa Waziri mwenye dhamana, Waziri wa Uchukuzi, Samweli Sitta wakati na mkutano wake na wandishi wa habari, alieleza kuwa Waziri Mkuu ameunda tume hiyo na inaanza kazi mara moja huku akiwataka madereva waache mgomo wao mara moja.
“Waziri Mkuu amewaita wamekahidi kwenda kuonana naye. Basi tunawaagiza madereva waache mara moja mgomo wao. Waziri Mkuu ameshaunda tume ya watu 13 kushughulikia matatizo yao wakiwemo viongozi hao wa madereva ambao watakuwa na haki sawa na wajumbe wengine wa serikali walioteuliwa na Waziri Mkuu” alieleza Sitta.
Sitta pia alimtaka Kamanda wa Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, kuwachukuliai hatua madereva wote watakaokahidi na kuendeleza mgomo.
Mwandishi Mwandamizi wa Modewji Blog, Andrew Chale akiwa eneo la tukio muda huu ndani ya kituo cha mabasi Ubungo kukuletea yote yanayoajiri usiku huu.
Hali ya kiza kinene ndani ya kituo cha Ubungi kama inavyoonekana huku miundombinu ikiwa mibovu kutokana na kuaribiwa na mvua, mwanza hafifu, unapatikana tu pindi gari hizo zinapowasha taa zao kama ilivyo hapa pichani.
Hii gari inayooneka pichani (kushoto) aina ya Noah ikiwa ikiwa imepakia abiria nje ya kituo cha mabasi Ubungo ambapo awali ilitangaza inaenda Morogoro!! Iligombewa kama njugu, lakini baadae wakabadilisha uamuzi huo na kuwashusha abiria wote, haikujulikana mara moja kilichosababisha kuwashusha abiria wote na kisha kuondoka zake bila kupakia kama ilivyokutwa na Camera yetu ya Modewji blog.