Paul Okoye wa Psquare akiwa na mtoto wake wa kiume, Andre (2) ambaye pia ameamua kumuingiza mtoto wake huyo kuwa ‘mnazi’ wa klabu ya Chelsea ambapo anamtabilia atakuwa mchezaji wa Kimataifa na wa kulipwa.
Na Andrew Chale, Modewji blog
Ukweli ni kuwa, wakali wanaotikisa katika muziki, kundi la Psquare linaloundwa na Mapacha ‘kaka wawili’ Peter na Paul Okoye (Psquare) ni wanazi wa kutupwa wa timu ya Chelsea Fc yenye makazi yake London huku ikitumia uwanja wa Arena, Stamford Bridge, Uingereza (UK).
Kwa ‘unazi’ huo umepelekea, Paul kumuingiza mtoto wake wa kiume kufuata mapenzi ya baba yake katika kuipenda, Chelsea. Mtoto wake huyo kiume aitwae Andre (2), amekuwa akipata mapenzi motomoto kutoka kwa wazazi wake tokea anazaliwa huku baba yake akifanya juu chini mtoto wake huyo anakuwa mwanasoka wa kimataifa.
Tayari Paul amemtengenezea njia mwanae huyo ikiwemo kumuingiza kwenye kituo cha soka akiwa ananolewa mara kwa mara kwa sasa huku akipenda awe nae karibu muda wote, licha ya ‘fans’ wake kupitia mitandao ya kijamii, ikiwemo Instagram, wakimtaka ampeleke, Stamford Bridge, UK, akajiunge na akademic ya soka, bado hajawa tayari kuonyesha hilo.
Paul ambaye anatumia IG ya RudeboyPsquare amekuwa akitupia picha mbalimbali za mtoto wake huyo, akimvesha jezi za Chelsea. Je! unadhani Paul atakuwa tayari kumpeleka mwanae huyo katika kituo cha soka cha klabu ya Chelsea?, Endelea kufuatilia mtandao huu kwani tutakuletea taarifa zaidi juu ya Paul na mwanae Andre kwani kwao wasanii hawa imekuwa tofauti, licha ya kuwa tumezoea, mtoto wa nyoka ni nyoka, kuwa mtoto angelithishwa muziki, lakini kwao hii imekuwa ni tofauti.
Tazama picha mbalimbali za mtoto wa Paul wa Psquare aitwae Andre katika pozi tofauti ambapo alianza kumpeleka kituo cha soka kuanzia ana mwaka mmoja hadi sasa.
Paul akiwa na Mwanae Andre, hivi karibuni
Mtoto wa Paul, Andre (2) akipooza koo baada ya mazoezi ya soka.
Andre akipasha misuli moto katika mazoezi yake ya soka.
Like Son Like Father…