Msemaji wa Jeshi la Rwanda Joseph Nzabamwita.
Jeshi la Rwanda limeituhumu nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kufyetua makusudi roketi kwenye eneo la mpaka.
Msemaji wa jeshi la Rwanda Joseph Nzabamwita, amesema kitendo cha kurushwa kwa roketi hilo kilikuwa ni cha uchokozi.
Tukio hilo limetokea wakati ambapo mapigano yamezuka tena mashariki mwa Kongo kwenye mji wa Goma, kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23, kundi ambalo linadaiwa kuungwa mkono na Rwanda.
Hata hivyo, Rwanda imekanusha madai hayo.
Mkuu wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo Martin Kobler amewaamuru wanajeshi wa kulinda amani kuwalinda raia.
Metoa agizo hilo baada ya bomu kushambulia mji wa Goma baada ya mapigano mapya kuzuka kati ya jeshi na waasi wa M23.