Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TMAA Bruno Mteta akitoa taarifa kwa waandishi wa habari jinsi wakala wa ukaguzi wa madini Tanzania ulivyoiwezesha serikali kukusanya mapato kutoka katika sekta ya madinikatika kipindi cha kuanzia 2009 hadi Machi 2013, ambapo amesema wakala huo umejipanga kendelea na ukaguzi wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini nchini ili kuhakikisha kuwa taifa linanufaika ipasavyo na rasilimali ya madini.
Aidha ametoa wito kwa wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano ili kuhakikisha majukumu ya wakala yanatekelezwa kikamilifu. Katikati ni Mkurugenzi Uthamini Madini na Huduma za Maabara Injinia Dominic Rwekaza na kulia ni Mkurugenzi wa Udhibiti na Ukaguzi wa Uzalishaji na Biashara ya Madini Injinia Liberatus Chizuzu.