Mabaki ya ajali iliyotokea maapema asubuhi ya leo inayoelezwa kuuwa watu 18 na kujeruhi 10 huko Ruaha Mbuyuni.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Hadi tunaendelea kuwapatia taarifa hizi usiku huu, tayari imeelezwa kuwa zaidi ya abiria 18, wameripotiwa kupoteza maisha huku 10 wakijeruhiwa vibaya katika ajali ya gari iliyotokea mapema leo majira ya asubuhi iliyohusisha basi la Abiria la Nganga lililogongana na lori aina ya Fuso uso kwa uso, hali iliyopelekea kuungua kwa magari hayo.
Awali taarifa kutoka eneo la tukio majira ya saa Nane mchana tuliripoti waliopoteza maisha ni abiria 6, lakini kwa sasa idadi hiyo imeelezwa kuongezeka na kwa sasa VIFO ni 18 huku zaidi ya 10 wakijeruhiwa vibaya Hii ni wa ajali iliyotokea mpakani mwa Morogoro na Iringa. TAARIFA ZAIDI TUTAENDELEA KUWAJUZA KADRI TUTAKAVYOZIPATA 0719076376/ Whatsapp0767076376.
Ajali Dodoma majira ya jioni ‘vifo zaidi kuripotiwa’
Gari aina ya Fuso lililokuwa limepakia watu kutoka msibani likionekana kuharibika vibaya baada ya kugongana naa kontena.
Habari zilizotufikia kwenye chumba chetu cha habari cha Modewji blog ni kuwa kuna ajaali mbaaya imeweza kutokea maeneo ya Ngilori na Tabu hotel huko Wilayani Gairo, Dodoma. Imeelezwa kuwa, ajali hiyo imehusisha lori aina ya Fuso iliyokuwa imepakia watu waliotoka msibani na gari kubwa aina ya semi trera na kugongana uso kwa uso.
Lori hilo linavyoonekana huku pembeni baadhi ya wananchi wakiangalia miili na majeruhi muda mfupi baad ya kufanya msaada huko Gairo, Dodoma jioni ya leo Aprili 12.
Hata hivyo, Idadi kamili ya watu waliopoteza maisha bado haijapatikana ila waliokaribu na tukio hilo wanaelezea kuwa ni ajali mbaya sana huenda vifo vikawa vingi zaidi hii ni taarifa ya Gairo, Dodoma kwa habari zaidi tutaendelea kukufikishia hapa.
Zaidi ya abiria 50 wanusurika kifo..basi lao lagongana uso kwa uso na lori la mafuta huko Tanga jioni ya leo
Basi la Burudani likionekana mara baada ya ajali hiyo kutokea huko eneo la Soni, jimbo la Bumbuli Mkoani Tanga.
Habari ambazo zimeweza kupatikana ni kuwa zaidi ya abiria 50 wamenusurika kifo baada ya basi lao lililojulikana kwa jina la Burudani, kugongana uso kwa uso na Lori la tenki la mafuta maeneo ya Soni katika jimbo la Bumbuli, mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa taarifa hizo ni kuwa, ilielezwa kuwa Lori la mafuta lilikata breki na kuvaana na basi hilo uso kwa uso. Kwenye ajali hiyo haakuna kifo ila inaelezwa kuwa abiruiiaa kadhaa wamejeruhiwa na wamekimbizwa Hospitali. Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi kila zinapopatikana kutoka vyanzo mbali mbali vya habari popote pale na kukujuza hapa zikiwa zimehaririwa na kukufikishia wewe msomaji wetu.
Asante endelea kuwa nasi, endelea kuperuzi nasi kila saa kila wakati.


