Basi la abiria la Nganga likionekana kuteketea kwa moto baada ya kugongana na Fuso majira ya saa mbili asubuhi leo Aprili 12, huko eneo la Ruaha Mbuyuni (Picha kwa mujibu wa mitandao ya kijamii).
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Chumba cha habari cha Modewji blog makao makuu kinaendelea kuwasiliana na vyanzo mbalimbali vya habari kutoka eneo la tukio la ajali mbaya iliyotokea mapema asubuhi ya leo Aprili 12 katika eneo hilo baada ya basi la abiria la Nganga linalofanya safari za Iringa na Ifakara kugongana lori aina ya Fuso.
Basi hilo (kulia) na Fuso (kushoto) yakionekana katika ajali hiyo.
Linavyoonekana basi hilo kwa sasa baada ya ajali hiyo….
Hadi sasa vyanzo vya ajali vinaeleza kuwa bado idadi ya vifo na majeruhi haijafahamika. Baada ya kugongana huko, magari hayo yote yaliwaka moto. (TAZAMA PICHA).
>>Chumba cha Habari Modewji blog kinaendelea kupokea taarifa zaidi hivyo pia kwa mwenye taarifa zaidi na picha anaweza kuwasiliana nasi kupitia namba hizi 0719076376 au whatsapp 0767076376