Waziri wa Kazi na Ajira nchini, Gaudensia Kabaka akiongea na madereva kwa kutumia kipaza sauti mapema mchana huu na kufuta baadhi ya vikwazo walivyokuwa wakivipinga madereva.
..Mgomo wadumu masaa 9..abiria waonja shubiri ya mabomu ya machozi
..Kamanda Kova, Waziri Kabaka ‘Mashujaa’ wamaliza mgomo ‘kiana’ Madereva wawasubiri Aprili 18
Andrew Chale wa Modewji blog
Hali ya mambo katika ‘segere’ la Madereva Nchini la kuweka mgomo baridi la kutoingia barabarani hadi hapo madai yao ya msingi yashughulikiwe, mgomo huo uliodumu kwa zaidi ya masaa nane, hatimaye umemalizika kiaina baada ya Serikali kuingilia kati na kutoa maazimio kadhaa yaliyopelekea madereva hao kurejea kwenye magari yao na kuanza safari hasa kwa mabasi yaendayo Mikoani na nchi jirani.
Kamanda Kova akiwasili katika eneo la Ubungo kwa ajili ya kuongea na madereva.
Modewji blog ambayo ilipiga kambi katika ‘segere’ hilo la mgomo huo wa madereva katika kituo cha Ubungo, huku wakishinikiza Mawaziri wenye dhamana kufika hapo na kuwafafanulia kero na madai yao sambamba na kuachiwa huru kwa baadhi ya madereva na viongozi wao zaidi ya sita (6) waliokuwa wakishikiliwa kwa madai mbalimbali ikiwemo hilo la kutatuliwa kero zao.
Madereva wakimsikiliza mmoja wa viongozi wao aliyekuwa akitoa neno la kuwataka madereva hao kuendelea kuwasubiria viongozi wa Serikali wafike kutoa majibu.
Mmoja wa viongozi wa Madereva aliyekuwa amekamatwa nakuachiwa na jeshi la Polisi, akiongea na wandishi wakati akiwahutubia madereva.
Hata hivyo majira ya saa tano (asubuhi) kamanda wa Kanda maalum Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda Suleiman Kova aliwasili na kuwatuliza madereva hao, lakini walimkatalia huku wakimwambia kwanza awaachie huru viongozi wao pamoja na baadhi ya madereva huku wakieleza kuwa, hawapo tayari hadi hapo viongozi wenye dhamana Mawaziri wafike mbele yao na wawahkikishie juu ya madai yao.
Kiongozi mwingine wa madereva ambaye naye alikamatwa na jeshi hilo na kuachiwa, akiongea na madereva kwa kutumia kipiza sauti
Baada ya zomea zomea ya madereva hao kwa Kamanda Kova, aliamua kuwaagiza maafisa wake wawachie huru viongozi hao na wafike nao hapo hali iliyotekeleza ndani ya dakika 15 na viongozi hao kufika na kuamsha shangwe kubwa kwa umati mkubwa wa madereva hao.
Baadhi ya madereva hao wakionekana kukataa baadhi ya kauli za viongozi walizokuwa wakitoa (Viongozi hawapo pichani) ambao walipiga kelele na kunyanyua mikono juu.
Viongozi hao walioachiwa waliamua kutoa maazimio yao kwa madereva wao na hali ya kutoelewana ilishindikana kabisa ndipo Kamanda Kova alipoamua kumpigia Waziri wa Kazi na Ajira, Mama Kabaka pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, waweze kufika kuongea na madereva hao.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Meck Sadik akiongea machache mbele ya madereva hao huku akiwa mpole kwa suala hilo kutomalizika kwa muda mrefu huku akiwahidi Serikali watalitolea ufumbuzi.
Viongozi waliwasili majira ya saa sita na nusu mchana na baadae baada ya majadiliano, wakarejea kwa madereva hao na kutoa matamko kadhaa.
“Malalamiko yenu nimeyasikia. Tutayafanyia kazi hivyo tupeni muda hadi hapo Aprili 18, tutapitia mikataba yenu na kero zote” alieleza Kabaka… Hata hivyo kauli yake hiyo ilisababisha kuzomewa kwa sauti na madereva wote huku wakimtaka atoe ufafanuzi wa madai yao zaidi ya mengi ikiwemo suala la kutokuwa na mikataba ya ajira.
“HATUNA MIKATABA RASMI YA AJIRA. KWA SAFARI TUNALIPWA Sh 30,000 hadi 40,000, hapo hapo tunaambiwa twende tukasome na kulipa sh Laki tano kama malipo ya mafunzo kwa chuo cha usafirishaji cha Taifa (NIT) kwa dereva wa ngazi ya PSV na mambo mengine.
Pia Jeshi la Polisi limezidi kuwapa adhabu kali ikiwemo kuwaandikia faini kila kukicha. Suala la Tochi kwa baadhi ya Polisi kugeuza mtaji hasa kwa kujificha hata sehemu isiyoruhusiwa.
Madai mengine ni pamoja na baadhi ya maaskari wa Usalama barabarani kuwa na tabia za kuwaandikia mara kwa mara makosa ya uongo na kulipishwa faini ambapo majina ya maaskari hao wameyakabidhi serikali.”
Baada ya madereva hao kusimamia msimamo wao huo kwa hoja.. huku wakipiga kelele kuwa hawataenda kuendesha magari mpaka hapo baadhi ya mambo ya msingi yafafanuliwe ikiwemo kutolewa kauli.
Mwandishi Mwandamizi na Mhariri wa Modewji blog, Andrew Chale akiwa kwenye tukio Ubungo ambaye alipiga kambi kituoni hapo kuanzia saa 11, alfajiri mapema leo.
..Waziri wa Kazi na Ajira, Kabaka aliamua ‘kujilipua’ kwa kusema:
“NAFUTA SUALA LA CHUO CHA USAFIRISHAJI CHA (NIT), MAMBO YOTE WALIYOKUWA WAKIWATAKA NYIE KUFANYA”
“Pia NAFUTA SUALA LA KULIPA LAKI TANO”.
“KUANZIA SASA MADEREVA WOTE MNATAKUWA NA MIKATABA YENU RASMI…KUANZIA SASA TUNAPITIA UPYA MIKATABA YA WAMILIKI WA MABASI YOTE HAPA NCHINI”… Baada ya kutolewa kauli hiyo na Kabaka madereva wote walishangilia huku wakiimba ‘MAMA! MAMA! MAMA!.
Waziri Kabaka akitoa kauli ya kusitisha vikwazo vyote dhidi ya madereva huku akiomba masuala yao mengine yatatolewa ufafanuzi hadi hapo Aprili 18.
Utamu huo wa madereva pia ulinogeshwa na Kamanda Kova, ambaye alisimama na kuwatangazia:
“NIMEFUTA FAINI ZOTE ‘MABAO’ KWA MADEREVA WOTE..KWA DEREVA ATAKAYEKAMATWA ANIPIGIE NAMBA 0754034224 AMA NJOO OFISINI KWANGU KUNISHITAKIA”
“NIMEFUTA SUALA LA TOCHI KWA MADEREVA.”
“SUALA LA ‘CHECK POINT’ ZOTE SASA NI KWA WAHALIFU NA MAJAMBAZI SI KWA MADEREVA TU”.
TUTAENDELEA KUWA NANYI NA JESHI LA POLISI LINAENDELEA KUSHIRIKIANA NA MADEREVA WOTE KWA TATIZO NAMBA YANGU HIYO MNIPIGIE!!…. Baada ya kauli hizo, Madereva waliamsha shangwe mbalimbali na kuanza kuimba KOVA! KOVA! KOVA! KOVA! Huku wakimfuata na kumpa mkono.
Hiyo ni majira ya saa saba na dakika 34.. ambapo baada ya hapo madereva hao walianza kulisukuma gari la Kamanda Kova hadi nje ya geti la Ubungo huku baadhi ya madereva wengine wakikimbilia kwenye magari yao na kupiga honi! Honi! Na abiria kwenda kupanda kwenye mabasi waliokuwa wameshakata tiketi na kuanza na safari.
Gari la kabisa kuondoka ndani ya standi kuu ya mabasi Ubungo ndio hiyoooo…. mambo taratibuuuuuu speed 20 hadi 30.. wamesema wakitaka wanaweza kuendesha speed hata 10.. ilimradi wafike… SASA HAKUNA TOCHI Mwendo wa kuteleza tu… byee byee poleni kwa mgomo abiria..
Dondoo muhimu:
Mwandishi wetu wakati wa mabomu hayo alikuwa kwenye hali mbaya huku kila mmoja akikimbilia anakokujua yeye kutokana na awali mgomo huo kuonekana wa kawaida, lakini ilipotimu majira ya saa tatu kasoro baadhi ya vijana wa wanaosadikiwa kuwa ni wa kihuni, walianza kufanya fujo, hali iliyopelekea Jeshi la Polisi kupiga mabomu ya machozi katika geti la kuingia na kutoka standi ya hiyo ya Ubungo.
Baadhi ya madereva wakionekana kwa mbaliiiii wakilisukuma gari la Kamanda Kova huku wakiimba ..KOVA! KOVA! KOVA!
Pia vijana hao na wapiga debe waliamua kuchoma moto matairi ya magari kwa shinikizo la kukataa baadhi ya magari yaliyokuwa yakianza kunyemelea abiria nje ya standi hiyo ya Ubungo. Modewji blog, ilishuhudia moja ya NOAH ikiranda randa nje ya kituo hicho hali iliyopelekea wapiga debe na vijana hao kuanza kupiga kelele za kutaka kuichoma moto kwani ilidaiwa kuwa ilitaka kubeba abiria kuwapeleka Tanga, hata hivyo ilinusurika kuchomwa moto kabla ya jeshi la Polisi kuingilia kati na kuanza kupiga mabomu hovyo (awali tulikuripotia kuwa NOAH imechomwa moto, Hivyo NOAH SI KWELI KAMA ILICHOMWA MOTO kutokana na NOAH hiyo iliweza kuporonyoka hasa kufuatia barabara kuwa ‘nyeupe’ pasipo foleni na kukimbia kusikojulikana na baadala yake walichoma tairi moto ilikuzuia magari mengine yasisogelee abiria..IFAHAMIKE HIVYO-Taarifa kamili).
Pichani ni baadhi ya Madereva waliachiwa ambao madereva wenzao walishinikiza waachiwe na waletwe mbele yao wawaone wakiwa wamewasili kwenye viwanja hivyo vya Ubungo.
Aidha, hadi hivi sasa baadhi ya mabasi ya jiji la Dar es Salaam, bado yapo machache barabarani huku baadhi yao wakiendelea kutoa huduma wakisaidiana na BODA BODA, pamoja na BAJAJI.
“Suala la leseni iliyokaa miaka mitatu kwenda kutakiwa kuibadilisha upya, ambapo malipo yao ni laki 5.
…Na huu ndio uliokuwa usafiri kwa muda wa masaa zaidi ya 6 kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, ambao walikuwa wakifanya safari zao baada ya daladala,mabasi ya mikoani na maroli kwa maddereva wao kugoma kwa kuanzia alfajiri hadi majira ya saa nane mchana baada ya viongozi wa Serikali kufuta baadhi ya madai yaliyokuwa yakitakiwa kuondolewa pamoja na kushughulikiwa kwa kero zao. (Picha zote na Andrew Chale wa Modewji blog 0719076376- UKINAKILI NA KUPAKUA PICHA WEKA ‘credit’ ya kwa msaada wa dewji blog.com).
Faini ya kuchelewa check pointi matrafiki wengi wanawalipisha faini kubwa wakati huo suala hilo Sumatra na Trafiki wanajichanganya kwenye sheria zao.
Suala la kutembea kwa mwendo wa speed 50, 80 na 120, suala hilo bado linashughulikiwa..