Msimamizi wa kituo cha watoto yatima cha Msimbazi Centre kilichopo jijini Dar es Salaam, Sister Anna Marandu (Kulia) akipokea msaada wa chakula na vifaa mbalimbali kwa ajili ya watoto wanaolelewa kituoni hapo kutoka kwa Meneja wa benki ya CBA tawi la barabara ya Nyerere, Nuru Mwangulangu wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho kutoa misaada mbalimbali na kucheza na watoto ikiwa ni moja ya shamrashamra za kuwapa burudani katika kipindi hichi cha Sikuu ya Pasaka.Wengine pichani ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo.
Watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Msimbazi wakifurahia zawadi mbalimbali zilizotplewa kwa ajili yao na benki ya CBA,waliosimama ni baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo ambao wametembelea kituo hicho kwa ajili ya kuitoa zawadi mbalimbali na kucheza na watoto ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea sikukuu ya Pasaka.
Baadhi ya wafanyakazi wa benki ya CBA wakiwa katika picha ya pamoja na msimamizi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Msimbazi kilichopo jijini Dar es Salaam. Sr.Anna Marandu na baadhi ya watoto wanaolelewa kituoni hapo muda mfupi baada ya kukabidhi msaada wa chakula na vitu mbalimbali kwa ajili ya kusaidia watoto hao ikiwa ni shamrashamra za kusherehekea sikukuu ya Pasaka.