Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam Suleiman Kova (kushoto).
Na.Mo Blog Team
Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalum ya Dar es Salaam kimeendesha operesheni mbalimbali za kukamata madereva na waendesha pikipiki (bodaboda) wasiotii sheria na kanuni za usalama barabarani.
Kufanyika kwa operesheni hiyo ni katika kuhakikisha kwamba sheria na kanuni za usalama barabarani zinasimamiwa na kufuatwa kikamilifu kwa nia ya kupunguza wimbi la ajali za barabarani.
Akitoa taarifa ya Kikosi cha usalama barabarani kanda maalum Dar es Salaam, Kamishna wa polisi kanda maalum Dar es Salaaam Suleiman Kova amesema kwa kipindi cha kuanzia tarehe 14 hadi 20. 08.2013 kikosi hicho kimekamata magari 1,388, makosa 2,272 na pikipiki 884 na jumla ya wapanda pikipiki 7 wamefikishwa mahakamani.
Amesema makosa yaliyolipiwa faini kwa ‘notification’ ni 2,260 ambapo jumla ya fedha zilizopatikana ni Shilingi 67,800,000/=.
Aidha amesema Operesheni hiyo inaendelea.