Mohamed Matumla Junior akimtupia makonde Mchina Wang Xiu Hua.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Bondia anayetoka kwenye familia yenye kusifika kwenye mchezo huo wa ngumi hapa Nchini Mohamed Matumla Junior usiku wa kuamkia leo Machi 28, ameweza kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania katika mchezo huo baada ya kumshinda bondia mwenzake kutoka China, Wang Xiu Hua katika pambano la kuwania ubingwa wa Super Bantam wa WBF Eliminator. Mchezo uliochezwa Ndani ya Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Katika mpaambano huo uliokuwa mkali na wa kuvutia kwa pande wa mabondia wote, ilimchukua dakika ya pili, makonde makali ya Matumla Jr, yalipelekea Mchina huyo kuomba ‘poo’ ili ajiweke vizuri baada ya kifaa maalum cha kuzuia eneo la chini kushuka mara kwa mara ‘yaani kikimpwelepweta’ hali iliyokuwa ikimlazimu mwamuzi wa pambano hilo kumzuia Matumla Jr asiendeleze makonde kwa Mchina ambaye alikuwa akipata kujiweka sawa.
Hali hiyo iliendelea zaidi ndipo ilipofika ‘round’ ya tano ambapo Mchina huyo licha ya kuonekana kuchoka aliweza kupokea makonde mengi kutoka kwa Matumla Jr, ambaye alikuwa akijaribu kutumia mkono wa kulia zaidi kuvurumisha makonde yake.
Hadi roundi ya 10 ya pambano hilo, lililokuwa la round 10, linamalizika, Mwamuzi wa Mpambano huo, Emmanuel Mlundwa aliweza kutangaza Matumla kushinda pambano dhidi ya Mchina, kwa pointi.
Kwa ushindi huo, Matumla anaenda Marekani kucheza katika pambano la utangulizi kwenye mpambano mkali na unaosubiriwa kwa hamu na wapenzi wengi wa masumbwi Duniani kati ya mabondia Floyd Mayweather, Jr. na Manny Pacquiao, Mei mwaka huu.
Japhet Kaseba akiwa chini baada ya kutandikwa masumbwi.
Aidha, katika mapambano ya utangulizi, Bondia Japhet Kaseba aliweza kugalagazwa vikali na bondia kutoka Mara, Maugo. Mchezo huo wa round 8, ulikuwa ni wa kuvutia, ambapo awali katika round ya 2, Kaseba alijaribu kumrushi makonde mpinzani wake, vilivyo, hata hivyo ndani ya dakika 6, Maugo aliweza kumpelekea masumbwi makali Kaseba na hadi kupelekea kuanguka chini ambapo hata hivyo hakuamka hadi madaktari walipofika kumuuliza kama ataendelea, ambapo mchezo uliichia hapo hapo kwa Maugo kuibuka mbabe.
Kwa upande wa pambano la mabondia wanawake, Bondia wa Tanzania, Asha Ngedere aliweza kuchezea kichapo kutoka kwa bondia mwenzake wa Kenya, baad ya kumdunda masumbwi makali hadi kwenda chini katika round ya 4, ya pambano hilo hali iliyopelekea Mkenya huyo kuibuka na ushindi na kuchukua taji.


