Msemaji wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Bw. Gaston Makwembe (kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari Mpango wa Halmashauri kujenga vituo vya Mabasi yaendayo mikoani na nchi za jirani katika maeneo ya Mbezi Luis na Boko Basihaya katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Meneja wa Kituo cha Mabasi Ubungo Bw. Juma Iddi (kushoto) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya ushiriki wao katika utoaji wa huduma ya usafiri wa Mabasi yaendayo haraka (Dar Rapid Transit-DART) katika mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Msemaji wa Halmashauri ya jiji Bw. Gaston Makwembe. (Picha na Eliphace Marwa).