Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mtoto mdogo wa Kitanzania mwenye IQ kubwa huyu hapa

$
0
0

10247290_791221147626346_6602541928733584586_n

Na Andrew Chale wa modewji blog

Huenda umesikia mengi juu ya watu wenye uwezo mkubwa wa kiakili na ufahamu hasa wa mambo ama IQ kubwa.

Kwa Tanzania mtoto mwenye IQ kubwa kwa  ni Mtoto Nice Valentino mwenye umri wa miaka 3, (Pichani) ameweza kuonesha uwezo mkubwa wa kukariri mambo.

kwa mujibu wa kituo cha Cloud FM cha Tanzania, kimenukuu maelezo kadhaa ikiwemo ya Baba  wa mtoto huyo, alieleza  kuwa, mtoto huyo alianza kuonesha uwezo tokea akiwa na miezi sita (mtoto mchanga) kwa kufanya vitu vilivyoonesha ishara ya uwezo wa jambo.

10952403_791221167626344_6142871847051780021_n

Miongoni mwa mambo ambayo yanafanya mtoto Nice kuwa na IQ  kubwa ni uwezo wake wa kuongea kiingereza kwa kuhesabu, kusoma na kufanya mambo kadhaa.

“Mtoto wangu ana uwezo wa kuhesabu kuanzia moja hadi 20, wakati hajasoma hata darasa moja. pia anaweza kuhesabu vitu vingi” alieleza baba huyo.

Mtoto huyo  Nice Valentino mwenye miaka 3 ametokea wilaya ya Kiteto mkoa wa Manyara. Hajasoma wala kufundishwa na yoyote ila anafahamu hesabu na anaongea Kiingereza tu.

Taarifa hii kwa msaada wa Cloud FM, kupitia kipindi cha Power Breakfast.

63961_791221200959674_2472470804513799395_n

11052511_791221184293009_2962062043417050372_n


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles