Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mashine ya BVR sasa haina tatizo hata kwa wenye vidole vyenye sugu – NEC

$
0
0

unnamed

Mbunge  wa  jimbo la  Ludewa, Mh. Deo Filikunjombe (kushoto) akiweka sahihi  katika mashine ya kielektroniki za Biometric Voters Registration (BVR),wakati akijiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura juzi katika kituo cha shule ya msingi Ludewa mjini, wa pili kulia anayeshuhudia ni kamishina wa tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC), Prof. Amone Chaligha.

Na MatukiodaimaBlog, Ludewa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema mchakato wa uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura  ulioanza kwa awamu ya  pili katika wilaya ya Ludewa mkoani Njombe umeanza  vyema na  sasa mashine hivyo za kielektroniki za Biometric Voters Registration (BVR), zinafanya kazi  vizuri hata kwa  wale  wenye vidole vyenye sugu.

Kauli  hiyo  imetolewa  jana na kamishina  wa  tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC)  Prof Amone Chaligha wakati akizungumza na  wanahabari  nje ya kituo cha kuandikishia  wapiga kura cha Ludewa Shuleni wilani  Ludewa mara baada ya  mbunge wa jimbo  la  Ludewa  Deo  Filikunjombe na msimamizi wa  zoezi  hilo wilayani Ludewa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo  kumaliza  zoezi la  kujinadikisha .

Alisema  kuwa kasoro za mashine za BVR ambazo awali zilikuwa zikisumbua  kutosoma alama za vidole  kwa baadhi ya watu hasa  wale  wenye sugu kwa  sasa kasoro  hizo  zimekwisha baada ya wataalamu wa mifumo ya Kompyuta kuzifanyia kazi ili  kufanya kazi kwa mazingira  yoyote yale .

Prof.Chaligha alisema kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha  wala  kuhofu  mashine  kutofanya kazi .

Alisema tokea zoezi hilo lianze wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.

“ Ni  kweli  siku  mbili tatu kasoro  za  sugu  katika  vidole  lilikuwa ni  shida  ila  wataalam wa IT  walilifanyia kazi na kwa  sasa  hakuna  kasoro kama  hizo na kuwa amepata  kuzungukia  vituo mbali mbali mjini Ludewa na  vijijini kasoro kama  hiyo haipo  tena kwa  sasa  hata  wakulima  wanajiandikisha bila shida   “

Kuhusu  kasi  ndogo  ya  uandikishaji  alisema  imechangiwa na waandikishaji  wenyewe kuwa na kasi ndogo na kuwa kimsingi  kila mwananchi  anapaswa  kujiandikisha kwa dakika 3 hadi 4  na  kuwa kwa  siku moja mashine  inauwezo wa kuandikisha  kiwango  cha chini kabisa ni kati ya  watu 50 -80

Hata  hivyo alisema  wanaofanya kazi  hiyo  ya uandikishaji  ni  wale ambao wanataaluma ya IT na  walifanyiwa mchujo na  wale  walioshindwa waliachwa  hivyo  wamejipanga  kuna kazi hiyo  inafanikiwa vilivyo.

Awali wakazi  wa Ludewa mjini  waliokutwa  kituoni  hapo  walielezea kero  kubwa ya  kukaa kwa muda mrefu  kituoni hapo  bila ya  kujiandikisha kwa madai ya  watoa huduma   hiyo  kufanya kazi kwa kasi ndogo  zaidi alisema mmoja kati ya  wakazi hao Bw  Ernest Yohana  .

Alisema  kwa upande wake  alifika kituoni hapo  toka majira ya saa 4 asubuhi na  kukaa kwenye foleni  hadi saa 9 ;30  alasiri  alipofanikiwa  kujiandikisha na kuwa kwao  wakulima  wanapotezewa  muda  mwingi .

Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo Filikunjombe ambae alifika  kujiandikisha akizungumza  mara  baada ya  kujiandikisha alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.

“Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho changu cha kupigia kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na mkanichagua kuwa mwakilishi wenu”,alisema Filikunjombe.

Hata  hivyo  aliipongeza  NEC kwa  kufanya kazi kwa ratiba  na  kuwataka  kuendelea  kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia  muda  zaidi  ili  kuwawezesha  wananchi  kwenda katika  shughuli  nyingine za uzalishaji mali.

Pia  alisema  kuwa  propaganda za  kuwa  vidole  vyenye  sugu mashine  haisomi   kuwa  hazina  ukweli kwani yeye  ni mbunge  mwenye sugu  katika  vidole pamoja na  wananchi wake  ila hakuna aliyelalamika  kushindwa  kujiandikisha  kwa ajili ya tatizo la  sugu .

Alisema kama mtanzania unapaswa kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba mwaka huu.

Filikunjombe aliyasema hayo katika kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.

Zoezi la  kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza tarehe 16/3/2015 litadumu katika  wilaya hiyo na nyingine kwa muda wa  siku saba kabla ya  kwenda  mikoa mingine ya  Katavi,Ruvuma,Lindi  na Mtwara .

zinafanya kazi  vizuri hata kwa  wale  wenye vidole  vyenye sugu.

Kauli  hiyo  imetolewa  juzi  na kamishina  wa  tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC)  Prof Amone Chaligha wakati akizungumza na  wanahabari  nje ya  kituo  cha kuandikishia  wapiga kura cha Ludewa Shuleni wilani  Ludewa mara baada ya  mbunge wa jimbo  la  Ludewa  Deo  Filikunjombe na msimamizi wa  zoezi  hilo wilayani Ludewa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo  kumaliza  zoezi la  kujinadikisha .

Alisema  kuwa kasoro za mashine za BVR ambazo awali zilikuwa zikisumbua  kutosoma alama za vidole  kwa baadhi ya watu hasa  wale  wenye sugu kwa  sasa kasoro  hizo  zimekwisha baada ya wataalamu wa mifumo ya Kompyuta kuzifanyia kazi ili  kufanya kazi kwa mazingira  yoyote yale .

Prof.Chaligha alisema kinachotakiwa ni wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwani zoezi hilo wilayani Ludewa litafanyika kwa muda wa siku saba na baada ya hapo zoezi litahamia maeneo mengine hivyo hakuna haja ya kuchelewa kujiandikisha  wala  kuhofu  mashine  kutofanya kazi .

Alisema tokea zoezi hilo lianze wilayani hapa hakuna kasoro ambazo zimejitokeza kama ilivyokuwa mji wa Makambako hivyo kila mwananchi anatakiwa kutumia fulsa hii ya kujipatia kitambulisho chake sasa ili kuweza kutumia katika upigaji kura.

“ Ni  kweli  siku  mbili tatu kasoro  za  sugu  katika  vidole  lilikuwa ni  shida  ila  wataalam wa IT  walilifanyia kazi na kwa  sasa  hakuna  kasoro kama  hizo na kuwa amepata  kuzungukia  vituo mbali mbali mjini Ludewa na  vijijini kasoro kama  hiyo haipo  tena kwa  sasa  hata  wakulima  wanajiandikisha bila shida   “

Kuhusu  kasi  ndogo  ya  uandikishaji  alisema  imechangiwa na waandikishaji  wenyewe kuwa na kasi ndogo na kuwa kimsingi  kila mwananchi  anapaswa  kujiandikisha kwa dakika 3 hadi 4  na  kuwa kwa  siku moja mashine  inauwezo wa kuandikisha  kiwango  cha chini kabisa ni kati ya  watu 50 -80

Hata  hivyo alisema  wanaofanya kazi  hiyo  ya uandikishaji  ni  wale ambao wanataaluma ya IT na  walifanyiwa mchujo na  wale  walioshindwa waliachwa  hivyo  wamejipanga  kuna kazi hiyo  inafanikiwa vilivyo.

Awali wakazi  wa Ludewa mjini  waliokutwa  kituoni  hapo  walielezea kero  kubwa ya  kukaa kwa muda mrefu  kituoni hapo  bila ya  kujiandikisha kwa madai ya  watoa huduma   hiyo  kufanya kazi kwa kasi ndogo  zaidi alisema mmoja kati ya  wakazi hao Bw  Ernest Yohana  .

Alisema  kwa upande wake  alifika kituoni hapo  toka majira ya saa 4 asubuhi na  kukaa kwenye foleni  hadi saa 9 ;30  alasiri  alipofanikiwa  kujiandikisha na kuwa kwao  wakulima  wanapotezewa  muda  mwingi .

Mbunge wa jimbo la Ludewa Bw Deo Filikunjombe ambae alifika  kujiandikisha akizungumza  mara  baada ya  kujiandikisha alisema kuwa kwa wananchi wa Ludewa vitambulisho hivyo vitatumika katika matumizi mbalimbali yakiwemo matumizi ya kusajilia simu na mengineyo hivyo hakuna haja ya kukaa kuwasikiliza wasio na mapenzi mema na nchi yao kwa kuwazuia wananchi kutimiza haki yao ya kikatiba.

“Mimi kama mbunge wajimbo la Ludewa leo nimejiandikisha na tayari nimesha kipata kitambulisho changu cha kupigia kura hivyo nawaomba wananchi wangu kujitokeza wote bila kukosa ili kuweza katika kufanikisha zoezi hili wani kitambuisho cha mpiga kura kitawasaidia kwa mambo mengi,msiwasikilize wazushi nisikilizeni mimi ambaye mliniamini na mkanichagua kuwa mwakilishi wenu”,alisema Filikunjombe.

Hata  hivyo  aliipongeza  NEC kwa  kufanya kazi kwa ratiba  na  kuwataka  kuendelea  kuifanya kazi hiyo kwa kuzingatia  muda  zaidi  ili  kuwawezesha  wananchi  kwenda katika  shughuli  nyingine za uzalishaji mali.

Pia  alisema  kuwa  propaganda za  kuwa  vidole  vyenye  sugu mashine  haisomi   kuwa  hazina  ukweli kwani yeye  ni mbunge  mwenye sugu  katika  vidole pamoja na  wananchi wake  ila hakuna aliyelalamika  kushindwa  kujiandikisha  kwa ajili ya tatizo la  sugu .

Alisema kama mtanzania unapaswa kujiandikisha na kutumia haki yako ya kikatiba katika kuipigia kura ya ndiyo katiba mpya inayopendekezwa pia kuchagua viongozi mnaowataka ifikapo oktoba mwaka huu.

Filikunjombe aliyasema hayo katika kituo cha uandikishwaji wapiga kura katika shule ya msingi Ludewa mjini wakati akijiandikisha ikiwa ni siku ya ufunguzi wa undikishwaji ulioanza rasmi wilayani hapa na kuwataka wananchi kuachana na maneno ya kizushi ya baadhi ya wanasiasa wanaowarubuni wananchi kutojiandikisha.

Zoezi la  kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura ambalo limeanza tarehe 16/3/2015 litadumu katika  wilaya hiyo na nyingine kwa muda wa  siku saba kabla ya  kwenda  mikoa mingine ya  Katavi,Ruvuma,Lindi  na Mtwara .

Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles