Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

SEMA Singida kutumia Milioni 80 kuwapiga msasa waratibu wa elimu mikoa ya Singida na Dodoma

$
0
0

DSC04523

Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Singida, Aziza Mumba, akizungumza kwenye ufunguzi wa mafunzo ya zana za ukaguzi na ufuatiliaji wa huduma za maji, elimu na usafi wa mazingira shuleni yaliyohudhuriwa na waratibu kata na walimu wakuu wa shule za msingi manispaa ya Singida. Kulia ni Meneja wa SEMA, Ivo  Manyanku na Kushoto ni mwenyekiti wa mafunzo hayo.

DSC04526

Baadhi ya waratibu na walimu wakuu wa shule za msingi manispaa ya Singida,waliohudhuria  mafunzo ya zana za ukaguzi na ufuatiliaji wa huduma za maji, elimu na usafi wa mazingira shuleni yaliyohudhuriwa na waratibu kata na walimu wakuu wa shule za msingi.(Picha na Nathaniel Limu).

Na Nathaniel Limu, Singida

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Sustainable Environment Management Action (SEMA) la mkoa wa Singida, linataraji kutumia zaidi ya shilingi 84 milioni kugharamia mafunzo kwa waratibu wa elimu kata  na walimu wakuu  341 wa mkoa wa Singida na Dodoma yanayohusu mwongo wa kitaifa wa maji,elimu ya afya na usafi wa mazingira katika shule za msingi na sekindari.

Hayo yamesemwa na Meneja wa SEMA, Ivo Manyanku,wakati akizungumza muda mfupi kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kaimu katibu tawala mkoa wa Singida, Aziza Mumba, kufungua mafunzo hayo yalinayohudhuriwa na waratibu elimu kata na baadhi ya walimu wakuu shule za msingi manispaa ya Singida.

Alisema kati ya waratibu elimu kata hao wanaoendelea kupewa mafunzo hayo,156 ni kutoka manispaa ya Singida na 185 ni wa mkoa wa Dodoma.

Ivo  alisema kuwa lengo au madhumuni ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waratibu hao, na walimu wakuu kuuelewa kwa kina mwongozo wa kitaifa,ili waweze kuusimamia vema utekelezaji wake.

“Naomba nitumie fursa hii kulishukuru shirika la WaterAid Tanzania kwa hatua yake ya kufadhili mafunzo haya na mradi wenyewe kwa ujumla.Pia nitumie nafasi hii kuiomba serikali na halmashauri za wilaya na manispaa,kuangalia uwezekano wa kuanza kutenga bajeti kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa vyoo bora,upatikanaji wa maji na usafi wa mazingira katika shule zake za msingi na sekondari”,amefafanua meneja Ivo.

Mgeni rasmi kaimu katibu tawala mkoa wa Singida,Aziza Mumba,alisema jitihada za kuongeza wanafunzi shuleni,zimeongeza mzigo mkubwa katika miundo mbinu ya shule iliyopo hasa katika huduma za maji,elimu ya afya na usafi wa mazingira.

“Takwimu zinaonyesha asilimia 38 tu ya shule nchini zina idadi ya kutosha ya vyoo,asilimia 20 zina mifumo ya usambazaji wa maji safi katika eno la shule zote nchini,asilimia chini ya 10 zina vifaa vya kunawia mikono vyenye maji wakati wote”,alisema.

Mumba alisema shule zisizo na mfumo wa maji safi,vifaa vya afya na usafi wa mazingira,zinaongoza kwa milipuko ya magonjwa ambayo huleta madhara katika mahudhurio na utendaji  nzuri kwa wanafunzi.

“Aidha,makundi yanayoathirika zaidi ni wanafunzi wa kike walio katika umri wa kubalehe na wanafunzi wenye ulemavu.Kimsingi hali ya kutokuwa na mazingira mazuri hulea na kukuza kizazi chenye tabia na desturi  mbaya ya afya na usafi wa mazingira”,alisema kaimu katibu tawala huyo.

Naye mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini hapa, Msafiri Msafiri, alisema kabla ya kuanzishwa kwa mradi huo wa ujenzi wa vyoo bora na shirika la SEMA,wanafunzi walilazimika kujipanga foleni kutokana  na miundo mbinu duni na uhaba wa matundu ya vyoo.Mbaya zaidi,baadhi yao walilazimika kujisaidia ovyo na hivyo kuchafua mazingira.

Mwalimu wa afya katika shule ya msingi Mahambe,Apaisaria Lyimo, alisema ili mwongozo wa kitaifa wa maji,elimu ya afya na usafi wa mazingira shuleni,uweze kufanikiwa katika shule zote,katika shule ambazo hazipo kwenye mradi  unaotekelezwa na HAPA, serikali inapaswa isaidie kujenga vyoo bora vinavyokidhi mahitaji yote na maji yawepo ya kutosha.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles