Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Soko la rangi kushuhudia mabadiliko kutokana na maendeleo mbalimbali ya miundombinu nchini

$
0
0

VIVA closeup Swahili+1

Kutokana na mpango mkakati wa serikali wa mwaka 2012 mpaka 2017 ambao unalenga upanuzi wa makazi katika mikoa mbalimbali, kumekuwa na ongezeko  kubwa la majengo ya  makazi, majengo ya ofisi na majengo ya masoko ambayo yameonekana  kuwa na manufaa na mchango mkubwa katika sekta mbalimbali na viwanda nchini Tanzania. Mpango huu wa upanuzi umejenga mahitaji kwa vifaa vya ujenzi ambapo kwa upande mwingine imeonekana kuwa ni faida kwa wauzaji ambapo wauzaji wengi wamekuwa na jitihada katika  kuongeza kasi  na namna ya uendeshaji na utoaji wao wa huduma ili kukabiliana na mahitaji mapya.

Kama ilivyo kwa saruji na vyuma, rangi pia imekuwa ni bidhaa kubwa na moja ambayo imekuwa ikihitajika sana kutokana na maendeleo ya miundombinu. Maendeleo haya ya kasi yamesababisha mabadiliko kwenye sekta ya rangi pia ili kukabiliana na mahitaji yanayojitokeza. Hii imesababisha kuanzishwa kwa teknolojia mpya, bidhaa na njia za kibunifu ili kukidhi mahitaji muhimu kwa ajili ya ubora unaoitajika.

Katika ulimwengu huu wa  teknolojia soko la rangi pia limekuwa likibadilika kuendana na maendeleo yaliyopo. Kumekuwapo na utumiaji wa mashine zinazotumia kompyuta ambazo  zimepunguza muda ufanyaji kazi na kuwa msaada mkubwa sana wasanifu na makandarasi wakiwa katika ujenzi.

Haya yameelezwa na Bw. Kishan Dhebar, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd. Moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Anasema kuwa “iwe  kwa ajili ya nyumba, biashara au viwanda soko la rangi nchini lipo katika hatua kubwa kutokana na maendeleo ambayo yanatokea hivi sasa. Sekta hii inaweza kusimama kutokana na mchango mkubwa inayoleta katika uchumi wa nchi”

Kampuni ya Insignia ni mfano wa kampuni ndogo ambayo imepitia mitihani mingi  na hatimaye imekuwa kiongozi na kuleta mabadiliko katika soko la  rangi nchini. Tangu kuanzishwa kwake mkoani Moshi (Kilimanjaro) kampuni hii sasa imeonyesha matunda yake. Bw Kishan pia ametoa maoni kwamba makampuni ya kisasa ya rangi kama vile Insignia hayana budi kudumisha ujasiriamali wake ambao umekuwa kama uti wa mgongo wa ukuaji wake. Na katika  maendeleo hayo vilevile anatoa wito wa kuwa na  “nia ya dhati na  ubunifu ambao utasaidia katika  ukuaji zaidi wa soko hilo. “

Kuanzia kwenye majengo ya makazi na majengo ya viwanda rangi inahitajika sana katika ujenzi wake. Miongoni mwa huduma mbalimbali zinazotolewa na Insignia ni pamoja na ‘THE ART’, inayotumika kulingana na mahitaji ya mteja.

Maendeleo ya makampuni kama vile Insignia kutoka biashara ndogo na kuwa kampuni kubwa ni ushahidi tosha katika soko la rangi kama moja ya sekta inayoshirikiana na sekta nyingine katika  kuchagiza uso wa miundombinu ya nchi yetu.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles