Wasomaji wa Mo dewji blog mnaoendelea kuperuzi mtandao huu ni kwamba taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii (Sio Mo dewji blog) zinazomuhusisha Mama Maria Nyerere. ‘SI ZA KWELI NA ZIPUUZWE’.
Awali habari mbalimbali juu ya kuenezwa kwa uvumi wa kifo kwa Mama Maria zilianza kusambaa hata kuzifikia chumba cha Habari cha Mo dewji, ambapo tumejiridhisha na kwa mujibu wa watu waliongea na familia ya Mama Nyerere, akiwemo Mtoto wake Madaraka Nyerere, alibainisha kuwa anaendelea vizuri.
Kwa msaada mkubwa akiwemo Maria Sarungi Tsehai aliyeweza kuongea na Madaraka Nyerere, juu ya kuenea kwa taarifa hizo, alimwakikishia kuwa, Mama Maria Nyerere ni mzima wa afya.
Maria Sarungi alitumia wasaha huo kukemia vikali tabia ya watu kuzushia watu kifo, kama hili kwani hata familia ya Nyerere imehudhunishwa sana.