Kiongozi wa kiroho wa kundi la ‘Muslim Brotherhood’ la nchini Misri Mohammed Badie amekamatwa mjini Cairo.
Taarifa zinasema kiongozi huyo amewekwa chini ya ulinzi katika nyumba moja ya makazi katika mji wa Nasr.
Hali ya tahadhari imetangazwa nchini Misri huku mapambano yakiendelea kufuatia msako unaofanyika kuwatafuta wapiganaji wa kiislam wenye msimamo mkali ambapo mamia ya watu wameuawa.
Takriban watu 900 wakiwemo polisi na wanajeshi 100, wameripotiwa kuuawa nchini humo tangu Jumatano, wakati jeshi lilipo tawanya kambi za maandamano zilizoundwa na wafuasi wa rais aliondolewa madarakani Mohammed Morsi, wengi wao wakiwa wanachama wa kundi la ‘Muslim Brotherhood’.
Siku ya Jumapili, waandamanaji 36 wa kiislam walikufa wakiwa katika gari la magereza katika mji mkuu wa Cairo.