Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyamapori nchini Tanzania ampongeza Rais Kenyatta

$
0
0

unnamed

Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Kidon Mkuu, akiwa Philipine Manila December 2014 kwenye harakati zake za matembezi ya kupinga kuuwawa kwa Tembo na Faru akiwa na wanaharakati wenzake wa huko Philipine.

unnamed (1)

Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini, Kidon Mkuu akiwa Philipine Manila December 2014 kwenye matembezi ya kupinga kuuwawa kwa Tembo na Faru akiwa na Susan Jaylo.

unnamed (2)

Mwanaharakati Kidon Mkuu akiwa kweye hoteli alikoshukia ya Sofitel mjini Manila Philipine.

Na Pamela Mollel, Arusha

Mwanaharakati wa siku nyingi wa wanyama pori na mazingira nchini Tanzania Bw.Kidon Mkuu amempongeza Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kwa kitendo cha kuchoma moto meno ya Tembo tani 15 katika kuhadhimisha siku ya wanyamapori Duniani.

Bw.Mkuu aliyasema hayo jana jijini Arusha wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu siku ya wanyamapori dunia, ambapo alisema kuwa anamuunga mkono Rais huyo kwa kufanya tukio hilo la kihistoria la kuchoma meno ya Tembo.

Alisema faida ya kufanya hivyo ni kudhibiti masoko na mianya ya kusafirisha meno hayo hali itakayosaidia ujangili wa Tembo kupungua.

Aidha alitoa wito kwa serikali na wizara kuhamasisha jamii kuhusu siku ya wanyamapori dunia kama wanavyofanya nchi zingine hali itakayosaidia jamii kufahamu wajibu wao wa kulinda wanyamapori.

Siku ya Wanyamapori Duniani ilitangazwa na Baraza la Umoja wa Mataifa Desemba 20, 2013 ili kuhamasisha kulinda wanyamapori na mapori na huadhimishwa tarehe3 April kila mwaka.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Latest Images

Trending Articles



Latest Images