Kutoka chumba cha habari cha modewjiblog , aliyekuwa Mkurugenzi wa TOT na Mbunge wa jimbo la Mbinga Magharibi, mkoa wa Ruvuma, Kapteni John Komba (pichani) amefariki dunia jioni hii katika hospitali ya TMJ Mikocheni jijini Dar alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.
Mtoto wake Jerry Komba amesema chanzo cha kifo chake ni Kushuka kwa Sukari akiwa nyumbani kwake Mbezi, na kumpeleka Hospitali ambako mauti yalimkuta.
Chanzo cha habari chetu kinasema taratibu za kuhamisha mwili wa marehemu kuupelea katika hopsitali ya Lugalo zinafanyika.
modewjiblog itaendelea kukupa habari zaidi hapo baadae.
modewjiblog inaungana na familia ya marehemu, Wana TOT pamoja na watanzania wote kuombeleza kifo cha Kapteni John Komba, Mungu awatie nguvu na faraja, familia ya marehemu katika kipindi hiki cha majonzi.
Bwana ametoa na Bwana alitwaa jina lake lihimidiwe Amen.