Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Waziri Kawambwa akwepa kuzungumza na wananchi waliovunjiwa nyumba zao kupisha ujenzi wa MUHANS.

$
0
0

SONY DSC

Mmoja wa kundi la Wananchi waliovunjiwa nyumba zao kupisha ujenzi wa  Chuo cha Afya cha Muhimbili (MUHANS)  akifafanua jambo kwa waandishi wa habari ambae hakutaka jina lake litajwe ambapo alisema “ Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Dk, Shukuru Kawambwa ameamua kutukimbia wakati anajua wazi kuwa tumekuja hapa ili atutatulie kero zetu lakini yeye anaamua kutokea mlango wa nyuma hivi kweli tunajenga taifa la namna gani kama waziri mwenye dahamana uaaogopa wananchi wake kuwapa ukweli”. Ambapo pia aliongeza kuwa mwezi wa Saba mwaka jana walilazimishwa kuvunjiwa nyumba zao bila kupewa taarifa mapema hatua iliyowafanya kwenda kwa Mkuu wa Mkoa ili kupatiwa ufumbuzi wa tatizo lao lakini mpaka hii leo bado hawajapatiwa maelezo ya kueleweka zaidi ya kuzungushwa kila kukicha.

Aliongeza kuwa “ Ndugu  Mwandishi sisi kama unavyotuona hapa toka asubuhi tupo hapa kwanza tuliambiwa twende Wizarani tulipofika Wizarani tukaambiwa Waziri hayupo ameenda katika mkutano huko viwanja vya Gymkhana na ndipo tukaamua kuja kumuona lakini mpaka sasa hatumuoni huyo Waziri”, alisema.

SONY DSC

Mkazi wa jiji la Dar Maria Daudi akilia kwa uchungu huku akisaidiwa na wasamaria wema nje ya ukumbi  wa mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam, Lengo la Maria ni kumtaka Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi  Dk, Shukuru Kawambwa atoke ili kumueleza shida yake, ambapo nyumba yake ilivunjwa kupisha ujenzi wa chuo cha Afya cha Muhimbili (MUHANS) huko Kibamba –Mlonganzilo.

SONY DSC

Maria Daudi akigaragara chini huku msamaria mwema akijaribu kumbembeleza na kumwinua.

SONY DSC

Mmoja  wa wananchi hao akionyesha moja ya nakala walizokabidhiwa ili kupatiwa malipo yao.

SONY DSC

Palikuwa hapatoshi full vilio.(PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles