Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, Eden Mahayo akisisitiza jambo wakati alipofika katika hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kukabidhi msaada wa vifa vya macho kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure. Kulia ni Mganga mkuu wa Wilaya hiyo Dkt.Francis Mwanisi,Kaimu Mkurugenzi wa Mkuranga Benjamin Majoya na Mratibu wa Taifa wa Huduma ya Macho Dkt.Nkundwe Mwakyusa.
Na Mwandishi Wetu
TAASISI isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision imetoa msaada wa vifaa vya kupimia macho wa zaidi ya sh milioni 11.4 kwa Wilaya za Mkuranga na Kibaha ziliyopo mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa msada huo , Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya hiyo Benjamin Majoya alisema msaada huo utasaidia katika kupandisha kiwango cha taaluma kwa wanafunzi katika Wilaya hiyo kutokana na idadi ya watoro darasani kupungua kuanzia mwaka huu.
Alisema kupungua kwa idadi ya wanafunzi watoro kutakwenda sambamba na kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi watakaojiunga na elimu yasekondari mwaka ujao.
Majoya alisema msaada uliotolewa na Taasisi hiyo umekuja kwa wakati mwafaka kwa wakati amabo ulikuwa ukihitajika hivyo mbali ya kuwasaidia wanafunzi wa shule za msingi lakini pia utawasaidia wananchi wote wa Wilaya hiyo.
Alibainisha kuwa msaada huo unaojumuisha mashine zote za kupimia macho pamoja kutengenezea miwani za aina mbalimbali utasaidia kuondoa tatizo la uoni hafifu ambalo hapo awali wazazi walikuwa na imani potofu kwamba huenda watoto wao wamerogwa.
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, Eden Mahayo (kushoto)akimkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Benjamin Majoya kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.
Akielezea ukubwa wa tatizo hilo ,alisema kuwa uoni hafifu umekuwa sababu ya mwanafunzi kutokufanya vizuri kitaaluma kutokana na kuugua mara kwa mara hivyo kusababisha utoro.
“Tunaishukuru sana Taasisi ya BrienHolden Vision kwa msaada waliotupatia na tunaahidi kuutumia kwaajili ya wananchi ,na ifahamikie kwamba hii itabaki kuwa mali ya hospitali ya Wilaya ya Mkuranga ’”alihitimisha Majoya.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Eden Mashayo alisema lengo la Taasisi yake ni kuwajengea uwezo wa kuona wanafunzi pamoja na walimu lakini pia kutoa mafunzo kwaajili ya walimu ili waweze kuwapima wanafunzi wapate huduma stahiki ili kuondokana na tatizo hilo.
Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Benjamin Majoya (kushoto) akikabidhiwa msaada wa vifaa vya macho na Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, Eden Mahayo kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambapo wanafunzi hao watapata huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafla hiyo ilifanyika katika hospitali ya wilaya ya mkuranga mkoa wa Pwani, wanaoshuhudia ni Mganga Mkuu wa wilaya hiyo Dkt.Francis Mwanisi, Mratibu mradi Rebecca Kasika na Mratibu wa Taifa wa Huduma ya Macho Dkt.Nkundwe Mwakyusa (wapili kutoka kushoto).
Mashayo aliahidi ushirikiano baina ya Taasisi yake ,Wizara ya Afya,Wilaya ya mkuranga na kwa kuleta mtaalamu wa masuala ya macho kila mwezi mara mbili ambaye atakuwa akiwahudumia wakazi wa eneo hilo ili kuondokana na tatizo la uoni hafifu ambalo litapungua kwa asilimia 10 .
Kwa upande wake Mkuu wa Mratibu wa huduma za macho Taifa kutoka Wizara ya Afya Dk Nkundwe Mwakyusa alisema kuwa mradi huo unaosaidia shule za Msingi bagamoyo na Kibaha umeshahudumia shule 121 katika awamu ya kwanza na awamu ya pili utahudumia shule 116 .
Akizungumzia changamoto zinazowakabili alisema kuwa huduma hizo hazipewi kipaumbele kwa sababu serikali inajua tu kunawafadhili .
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, Eden Mahayo (kushoto) akimuonyehsa mashine ya kutengenezea miwani baada ya kumkabidhi msaada wa sanduku la vifaa vya kupimia macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Benjamin Majoya kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambao watanufaika na huduma ya kupima na kutibiwa macho bure. hafla hiyo ilifanyika katika hospitali ya Wilaya hiyo.kulia ni Mratibu huduma za macho Mkuranga Dkt.Gilbert Mrema.
Hata hivyo alibainisha kuwa ili kutatuua changamoto hizo na kuifanya jamii iwe na uelewa sahihi juu ya magonjwa ya macho mikakati iliyopo huenda mambo yakabadilika na mwaka huu jamii itaanza kupata taarifa sahihi kuhusu magonjwa ya macho.
Naye daktari Mtalamu wa macho, Gilbert Massawe wa hospitali ya wilaya ya Mkuranga na Afisa Maendeleo ya jamii mji wa kibaha Leah Rwanji waliishukuru Wizara ya Afya sambamba na Taasisi ya
Brien Holden Vision kwa msaada wao na kubainisha kuwa utasaidia kupunguza idadi ya utoro kwa wanafunzi kwa asilimia 10.
Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Kaimu Benjamin Majoya (kulia) Mganga Mkuu wa Wilaya ya hiyo Dkt,Francis Mwanisi akionyeshwa mashine ya kupimia macho mara baada ya kuwakabidhi vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambao watanufaika na huduma ya kupima na kutibiwa macho bure.hafla hiyo ilifanyika katika hospitali ya Wilaya hiyo.
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, Eden Mahayo (kushoto) akimuonyesha Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Benjamin Majoya (kulia) moja ya miwani iliyotengenezwa na taasisi yake wakati wa hafla ya kumkabidhi vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambao watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho na matibabu bure.
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, Eden Mahayo (kushoto) akijaribu kumpima miwani matroni wa Hospitali ya Mkuranga Rosemary Magombola wakati wa hafla ya kumkabidhi wa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wa shule za msingi 122 za Mkuranga ambao watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho pamoja na matibabu bure. Mkurugenzi wa manispaa ya Mkuranga Kaimu Benjamin Majoya (kulia) Mganga Mkuu wa Wilaya ya hiyo Dkt,Francis Mwanisi.
Matroni wa hospitali ya wiraya ya Mkuranga, Rosemary Magombola akisoma moja ya maneno kwenye kibao maalumu cha kupimia macho mara baada ya kukabidhiwa msaada huo na taasisi isiyo ya kiserikali ya Brien Holden Vision Institute kwa ajili ya wanafunzi wa shule za msingi 122. Kulia ni Mratibu wa taifa wa huduma za macho Dkt.Nkundwa Mwakyusa (kushoto) Mratibu wa mradi huo kwa watoto wa shule za msingi toka taasisi ya Brien Holden Vision Institute, Rebecca Kasika.
Afisa maendeleo ya jamii ya mji wa Kibaha mkoa wa pwani akikabidhiwa na Mashine ya kupimia macho na Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, Eden Mahayo (kulia) wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuwahudumia wanafunzi wa Wilaya hiyo ya Kibaha ambao watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho pamoja na matibabu bure.
Afisa Mkazi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, Eden Mahayo (kushoto) akisisitiza jambo kuhusiana na utunzaji wa vifaa vya kupimia macho mara baada ya kuwakabidhi msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuwa hudumia wanafunzi wa shule za msingi za Kibaha mkoani Pwani ambao watanufaika na huduma hiyo ya upimaji macho pamoja na kupatiwa matibabu bure.
Wafanyakazi wa hospitali ya Kibaha kitengo cha macho wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Brien Holden Vision Institute mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4.
Wafanyakazi wa Hospitali ya Mkuranga wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa taasisi isiyo ya Kiserikali ya Brien Holden Vision Institute, mara baada ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya macho vyenye thamani ya shilingi milioni 11.4 kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi wa shule za msingi ambao watanufaika na mradi huo bure.