Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Viongozi wauwaga mwili wa marehemu Salmin Awadh Salmin Baraza la Wawakilishi

$
0
0

DSC_0157

Waziri Mkuu mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Edward Lowassa akiingia katika ukumbi wa baraza la wawakilishi kuuwaga mwili wa aliekuwa Mwakilishi wa Jimbo la Magomeni Marehemu Salmin Awadh Salmin aliefariki ghafla jana. (Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).

DSC_0176

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakiingia katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi  kuuwaga mwili wa Marehemu Salimn Awadh.

DSC_0201

Mwili wa Marehemu Salmin Awadh  ukiingizwa  katika Ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani kwa ajili ya kuagwa rasmi.

DSC_0218

Viongozi mbali mbali  wakijumuika na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakitoa heshma za mwisho kwa marehemu Salmin Awadh Salmin katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani.

DSC_0276

Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji akiongoza  waumini katika Sala ya Marehemu Salmin Awadh Salmin katika Masjid Noor Muhammad (SAW) uliopo Mtaa wa Kwamchina mwanzo.

DSC_0288

Viongozi mbali mbali akiwemo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Muhammed Shein wakimuombea dua Marehemu Salmin Awadh baada ya sala iliyofanyika Masjid Noor Muhammad (SAW).

DSC_0290

Viongozi walioshiriki sala ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiagana baada ya kumalizika sala hiyo.

DSC_0296

 Naibu Katibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai  na Mwakilishi wa Jimbo la Kikwajuni Mahmoud Muhammed wakibadilishana mawazo kuhusu msiba huo.

DSC_0309

Mamia ya wananchi waliohudhuria sala ya kumuombea Marehemu Salmin Awadh Salmin wakiutoa msikitini mwili wa marehemu kuelekea kijijini kwao Makunduchi kwa mazishi.

DSC_0311

Msafara uliobeba mwili wa Marehemu Salmin ukiondoka Masjid Noor Muhammad (SAW) kuelekea Makunduchi kwa ajili ya mazishi.(Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles