Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Nne wa PSPF baada ya kufangua mkutano huo kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi Tuzo Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Rasirimaliwatu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Ernest Maalugu, ikiwa ni heshima kwa wizara hiyo kutokana na umakini wa hali ya juu katika kuwasilisha makto ya michango ya watumishi wake kwa Mfuko wa PSPF na utoaji wa taarifa sahihi na kwa wakati za watumishi wake kwa mfuko huo.. Makabidhiano hayo yalifanyika wakati Waziri Mkuu alipofungua Mkutano wa Nne wa Mfuko wa PSPF mjini Dodoma Februari 18, 2015. Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF, George Yambesi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, Naibu Waziri wa Fedha, Adam Malima, na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka.(Picha na Ofisi ya Waziri MKuu).
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Fao la uzazi la Mfuko wa PSPF wakati alipofungua mkutano wa nne wa PSPF kwenye Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015. Kulia ni Waziri wa Kazi na Ajira Gaudencia Kabaka na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Fedha Adam Malima. Wapili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa, watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Maingu na wanne kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya PSPF, George Yambesi.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na watumishi wa Benki ya NMB waliokuwa wakionyesha shughuli mbalimbali za Benki hiyo kwa washiriki wa Mkutano wa Nne wa PSPF uliofanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Nne wa PSPF wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua mkutano wao kwenye Kituo cha Mkutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015.
Wasanii wa kikundi cha Mchoya cha Dodoma wakitumbuiza katika mkutano wa Nne wa Mfuko wa PSPF uliofunguliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiki wa mkutano wa nne wa mfuko wa PSPF alioufungua kwenye Kituo cha Mikutno cha Saint Gaspar mjini Dodoma Februari 18, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).