Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Rais wa Ujerumani kuzuru Zanzibar

$
0
0

330

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitembelea Bandari ya Malindi kuangalia matayarisho ya ujio wa  Rais wa shirikisho la Ujerumani Bwana Joachik Gauck.. Kushoto kwa Balozi Seif ni Mshauri wa Rais anaesimamia Uchumi, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Moh’d Ramia na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar Nd. Abdulla Juma Abdulla.

Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck anatarajiwa kuwasili Zanzibar kesho asubuhi kwa kufanya ziara ya kutwa moja akitokea Mjini Dar es salaam.

Bwana Joachim atapokelewa na Mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein, Mawaziri wa Serikali, Viongozi wa Kisiasa na baadhi ya raia wa Ujerumani waliopo Zanzibar huko Bandari ya malindi Mjini Zanzibar.

Matayarisho ya mapokezi ya ujio wa Kiongozi huyo wa Shirikisho la Ujerumani yamekamilika ambapo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alipata wasaa wa kufika Bandari ya Malindi kukagua matayarisho hayo.

Mshauri wa Rais wa Zanzibar  anayesimamia Uchumi, Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Moh’d Ramia Abdiwawa alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba hatua zote zilizopangwa kuchukuliwa katika matayarisho hayo zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa.

333

Balozi Seif akiwa na Viongozi wa Kamati ya kuratibu Mapokezi ya Rais wa Ujerumani wakirudi kukagua eneo la kushukia boti  ziendazo kwa kasi katika Bandari ya Malindi. Kushoto kwake ni  Mshauri wa Rais Balozi Moh’d Ramia, Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji pamoja na Mkurugenzi Bandari Nd. Abdulla Juma.

Balozi Ramia alisema Mgeni huyo anatazamiwa kuwasili kwa Boti iendayo kwa Kasi ya Kilimanjaro wakati wa asubuhi na kupata fursa ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed  Shein Ikulu Mjini Zanzibar.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Zanzibar Balozi  Silima Kombo Haji alimueleza Balozi Seif kwamba utaratibu maalum umeandaliwa kwa Viongozi  wenyeji waliopangwa kumpokea Kiongozi huyo.

Balozi Silima alisema maafisa wa Itifaki watakuwepo Bandarini hapo kwa lengo la kuwaelekeza Viongozi wote waliopangwa kufika eneo hilo kwa shughuli hiyo muhimu ya Kimataifa.

335

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa pamoja na Balozi Mdogo wa Heshima wa Shirikisho la Ujerumani hapa Zanzibar Balozi Has –Dieter Allgaier wakielekea kukagua chumba  cha watu Mashuhuri { VIP }  kiliopo Bandari ya Malindi ambacho kimewekwa akiba kwa ujio wa Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck.

Akitoa shukrani zake  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alielezea kuridhika kwake na hatua za maandalizi hayo na kuipongeza Kamati maalum iliyoundwa ya kuratibu mapokezi hayo.

Rais wa Shirikisho la Ujerumani Bwana Joachim Gauck awapo Zanzibar pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na Viongozi wa Kidini katika Hoteli ya Serena iliyopo Forodhani Mjini Zanzibar.

Bwana Joachim anatazamiwa kuondoka  Zanzibar kupitia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume  Zanzibar wakati wa jioni kuekelea Mkoani Arusha kumalizia ziara yake Nchini Tanzania.

343

Mshauri wa Rais anayesimamia Uchumi,Uwekezaji na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Moh’ d Ramia akimuelezea Balozi Seif hatua zilizochukuliwa katika matayarisho ya ujio wa Rais wa Ujerumani. Kati kati yao ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d na kulia ya Balozi Ramia ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo Haji.(Picha na – OMPR – ZNZ).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles