Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

KINANA amaliza ziara yake mkoa wa mjini magharibi Zanzibar

$
0
0

unnamed

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi dawa kwa mganga mkuu wa hospitali ya jimbo la Mpendae Dr. Omar Shaban Amran wakati alipokabidhi sehemu  ya madawa kwa hospitali hiyo ambayo yametolewa  na mbunge wa jimbo la Mpendae Mh. Salum Turki kiasi cha makontena ya dawa  manne yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja  na pointi Nne yatakayosaidia katika hospitali zote za Zanzibar, Kinana akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi amemalizia ziara yake leo katika mkoa wa  Mjini Magharibi wilaya ya Amani jimbo la Mpendae kabla ya kuendelea na ziara mikoa mingine ya Zanzibar.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-ZANZIBAR).

unnamed (1)

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya ukarabati wa barabara kwa kusambaza kifusi katika barabara inayounganisha  hospitali ya Jimbo la Mpendae na Barabara kuu ya Mchina.

unnamed (2)

Mh. Silima Borafya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi naye akishiriki katika ukarabati huo.

unnamed (3)

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikiwa ameshikilia toroli huku mbunge wa jimbo la Mpendae Mh. Salum Turki akijaza kifuzi katika toroli hilo wakati Ndugu Abdulrahman Kinana aliposhiriki ukarabati wa barabara hiyo.

unnamed (4)

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua ofisi ya CCM tawi la Kilimahewa juu ambalo lilichomwa na wafuasi wa Uamsho wakati wa vurugu hizo mwaka juzi.

unnamed (5)

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza mbunge wa jimbo la Chumbuni Mh. Pereira Silima wakati akizungumza katika tawi la Kiungani ambalo lilitembelewa na Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana.

unnamed (6)

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya utandazaji wa mabomba ya mradi wa maji SEMUSO katika kijiji cha Wazee cha mjini Zanzibar. 

unnamed (7)

Mbunge wa jimbo la Chumbuni Mh. Pereira Silima akiwa na viongozi wengine wa CCM katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Bint Amran Mpendae wilaya ya Amani.

unnamed (8)

Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akijumuika na viongozi hao wakati wa mkutano wa hadhara.

unnamed (9)

Mlezi wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Shamsi Vuai Nahodha akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Bint Amrani jimbo la Mpendae.

unnamed (10)

Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akipiga nondo katika mkutano huo.

unnamed (11)

Inaonyesha wameikubali Katiba inayopendekezwa kwa jinsi walivyo nyoosha mikono yao juu.

unnamed (12)

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Mzee Silima akitema cheche zake.

unnamed (13)

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar wa CCM Ndugu Vuai Ali Vuai akiwafafanulia wananchi  faida za katiba mpya inayopendekezwa. 

unnamed (14)

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi katika mkutano huo.

unnamed (15)

Umati wa watu waliohudhuria ukifuatilia mambo muhimu yaliyokuwa yakielezwa na Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles