Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mwanahabari Humphrey Kisika atangaza kumvaa Kayombo mbunge wa Mbinga Mashariki katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

$
0
0

ggggggggggg

Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Humphrey Kisika (32).

Na Fredy Mgunda

Katika kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika octoba mwaka huu Afisa Habari na Mahusiano wilaya ya Iringa Hafley Kisika ametangaza kugombea ubunge katika jimbo la Mbinga mashariki kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM, ili kuleta maendeleo katika jimbo hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari KISIKA amesema kuwa sababu inayompelekea kugombea ubunge katika jimbo hilo ni pamoja na kuleta siasa safi pia kuunganisha wananchi na wataalamu mbali mbalimbali ili kusaidia jimbo hilo kuendelea hasa katika maswala ya miundombinu.

Aidha amesema kuwa chama cha mapinduzi kina sera nzuri na kwamba ushirikishwaji wa makundi mbalimbali ikiwamo vijana,wazee na makundi mengine katika jamii kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua jimbo la Mbinga mashariki kimaendeleo.

KISIKA amekanusha uvumi unaodai Chama cha Mapinduzi kimepoteza dira na kuongeza kuwa CCM ni  chama imara na kuwataka vijana watambue wanafanya nini na kuwa mstari wa mbele kuleta mabadiliko ya kimaendeleo  na sio kuleta machafuko.

Ameendelea kusema kuwa pamoja na kuwa na ushindani mkubwa katika siasa lakini ilani na sera za chama husika pamoja na mgombea ndizo ambazo zinaweza kumtambulisha mtu kama anauwezo wa kuwa kiongozi.

Hata hivyo KISIKA anatarajia kugombea ubunge katika jimbo la Mbinga mashariki huku akiwa ni mjumbe wa chama cha mapinduzi katika chuo kikuu cha Tumaini,Mbunge kwa miaka mitatu pamoja na katibu katika kamati mbalimbali chuo kikuu cha Tumaini mbali na hayo KISIKA ni Afisa Habari katika halmashauri ya wilaya ya Iringa.

Kwa vyovyote iwavyo, mapigo ya moyo ya Mbunge wa Jimbo la Mbinga Mshariki mkoani Ruvuma, Gaudance Kayombo yataongezeka mara dufu baada ya kijana msomi; Afisa Habari wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, Humphrey Kisika (32) kutangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.

Kisika, msomi mwenye shahada ya kwanza ya uandishi wa habari ambaye pia ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, anayesoma shahada ya pili ya uandishi wa habari na utawala anataka kuwania nafasi hiyo kupitia chama chake Chama cha Mapinduzi (CCM).


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles