Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Ali Kiba azindua Video yake mpya “MWANA” kua wa kwanza kuiona hapa

$
0
0

Untitled

Akiwa ana nyimbo za “Mwana” na “Kimasomaso” zikiongoza  katika vituo mbali mbali Africa, Alikiba aachia video ya “Mwana” iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu jana ,Ijumaa tarehe 19 Decemba 2014 kwa mamilioni ya mashabiki Africa na duniani. “Mwana” ni nyimbo ya kwanza  baada ya kufunga mkataba wake na kampuni ya Rockstar4000 Management na Rockstar Publishing.

Rekodi ya “Mwana” ni nyimbo ya kwanza kutoka kwenye albamu ya tatu ya Alikiba baada ya kutokuwa katika muziki kwa muda wa miaka mitatu. Alikiba alifafanua kwa kusema “ Hii ni album itayoonyesha kukua kwangu kimuziki na kuonyesha utofauti mbali mbali katika kipaji changu nilichojaliwa.” 

Alikiba alitoa kibali ili video ya “Mwana” iruke hewani jana “exclusively” kwa masaa 24 kwenye vituo vya televisheni vitano Africa katika vipindi maarufu kwenye vituo hivyo na kuwafikia mashabiki zaidi ya milioni 500 kwa pamoja. Vituo vya televisheni hivyo ni Clouds TV kuonyesha exclusive Tanzania, Nation TV kuonyesha exclusive Uganda, One Music Networks kuonyesha exclusive Cameroon, Angola, Ethiopia, USA na UK, Sound City kuonyesha exclusive Nigeria na Ghana na Citizen TV exclusive kwa upande wa Kenya, DRC Congo na Rwanda

Mashabiki wanaweza kuangalia video ya “Mwana” katika Youtube channel yake Alikiba au hapa

Au kwa kupitia mitandao yake ya kijamii.

Video ya “Mwana” itaendendelea kuruka kwenye vitu vingine mbali mbali Africa na duniani leo

Alikiba’s official website: www.IamAlikiba

Bookings: officialalikiba@gmail.com

Facebook: www.facebook.com/rockstar.alikiba

Twitter: @OfficialAlikiba or twitter.com/officialalikiba

Instagram: @OfficialAlikiba or instagram.com/officialalikiba

YouTube: https://www.youtube.com/channel/UCSlyAXLzVNfsh3geYD9Cc4A


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles