Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Willy Kitima ateuliwa kuwa msaidizi wa Rais-nyaraka

$
0
0

Ikulu-tz

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bwana Willy Kitima kuwa Msaidizi wa Rais – Nyaraka (Documentation) kuanzia Alhamisi iliyopita, Desemba 11, 2014.

Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kitima alikuwa Mratibu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa ya Biashara nchini ya Business Action Against Corruption (BAAC) Tanzania.

Taasisi hiyo inaendeshwa kwa ushirikiano kati ya Jumuiya ya Madola na Serikali ya Tanzania kupitia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (PCCB) na Taasisi ya Uendelezaji Sekta Binafsi nchini ya PPSF.

Bwana Kitima pia amewahi kuwa Mkrugenzi Mtendaji wa Shirika la Kufutilia Nyendo za Rushwa Kimataifa la Transparency International (TI) nchini. Aidha, ana ujuzi wa shughuli za benki na vyombo vya habari.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

Ikulu,

DAR ES SALAAM. 

17 Desemba, 2014


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles