Pichani askari Polisi wakiwa eneo la tukio kwa ajili ya kuubeba mwili wa Marehemu ERASTO MSUYA.
Mfanyabiashara maarufu wa madini na mmiliki wa hoteli ya SG RESORT na MEZZALUNA mkoani Arusha Milionea ERASTO MSUYA ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana mchana huu eneo la KIA akitokea Mererani kuelekea Moshi.
Polisi wanaendelea na uchunguzi baada ya kuuchukua mwili wa marehemu kutoka kwenye eneo la tukio na kuupeleka hospitalini.
Mwili wa marehemu upo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Bomang’ombe.
MO BLOG itaendelea kukupa updates ya taratibu za mazishi ya marehemu.
WADAU KUMRADHI KWA PICHA HII KAMA ITAKUKWAZWA. Mwili wa Marehemu ERASTO MSUYA ukiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti Boman’gombe ukiwa na majereha pamoja na matundu ya risasi kifuani.
Mwili wa marehemu EARSTO MSUYA ukiwa umelazwa mita chache karibu na gari lake baada ya tukio.