Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Silaa jana amehudhuria maadhimisho ya siku ya UKIMWI iliyoadhimishwa na manispaa ya Ilala kwenye kata ya Vingunguti ambapo ametumia fursa hiyo kuhamasisha wanaume kupima VVU kwani takwimu zinaonyesha asilimia ndogo ya wanaume wanajitokeza kupima.
Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akizungumza na mtoa huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa VVU wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani.
Mtoa huduma ya ushauri nasaha na upimaji wa VVU akichukua vipimo vya damu kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani iliyofanyika katika kata ya Vingunguti.