Mwenyekiti na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Viwanda vya Dangote (Dangote Industries Group), mfanyabiashara maarufu Afrika, Alhaji Aliko Dangote akitumia gari kukagua maendeleo ya ujenzi wa kiwanda chake kikubwa cha saruji katika Kijiji cha Msijute, mkoani Mtwara leo.
Ndege ya bilionea huyo wa Afrika, Alhaji Dangote ikitua kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara
Alhaji Aliko Dangote kutoka Nigeria, akilakiwa na Mwakilishi Mkazi wa Dangote nchini, Esther Baruti alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara leo. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)
Balozi wa Nigeria nchini, Dk. Ishaya Manjanbu akimlaki Alhaji Dangote.
Alhaji Dangote akiwa na maofisa wake katika kikao na viongozi wa kampuni inayojenga kiwanda hicho ya Dil & Sinoma kwa ajili ya kupewa maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho ambacho kitakuwa cha tatu kwa ukubwa Afrika.
Waandishi wa habari wakimhoji Dangote kuhusu maendeleo ya ujenzi wa kiwanda hicho.
Alhaji Dangote akiwa kwenye msafara wa magari akikagua maendeleo ya ujenzi ya kiwanda cha saruji Mtwara.
Mwakilishi Mkazi wa Kampuni hiyo ya Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiwa na mmoja wa wakurugenzi wa Kampuni ya Dangote
Alhaji Dangote akisindikizwa kwenda kupanda ndege kwenda nchini Ethiopia kuendelea na ziara yake
Ofisa Mnadhimu wa Poilisi Mkoa wa Mtwara, George Salala akiagana na Alhaji Dangote
Alhaji Dangote akipanda ndege tayari kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Mtwara.
Mwakilishi Mkazi wa Dangote hapa nchini, Esther Baruti akiondoka baada ya kuagana na Dangote
Ndege iliyombeba Alhaji Dangote ikipaa