Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye (katikati) akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa “Oxygen Flow meters” kwa uongozi wa Hospitali ya Mwananyamala. Kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyalama Dr. Sophinias Ngonyani na kulia ni Mkuu wa Fedha ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Bw. Gofrey Ndalahwa.(Picha na Zainul Mzige wa Dewji Blog).
Na. Mo Blog Team.
Benki ya KCB Tanzania leo imekabidhi vifaa kwa uongozi wa hospitali ya Mwananyamala ambavyo ni Oxygen Flow Meters vyenye jumla ya thamani ya shilingi milioni 7.2.
Akikabidhi vifaa hivyo Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye amesema huu ni mwaka wa pili mfululizo ambapo benki hiyo inatoa msaada kwa hospitali ya Mwananyamala, ambapo mwaka jana ilitoa vitanda 65 vikiwemo 660 na loka zake kwa ajili ya wadi ya kinamama na vitano kwa ajili ya kujifungulia, ambavyo vyote vilikuwa na thamani ya shilingi 45,000,000/=.
Ameongeza kusema kuwa mwaka huu wametenga kiasi kikubwa zaidi cha fedha kwa ajili ya kusaidia jamii inayowazunguka kupitia sekta ya Afya, Elimu, Mafunzo kwa Wajasiriamali wadogo na wa kati(SMEs na Sekta isiyo rasmi (jamii yenye shida mbalimbali kama vyakula na maafa.
Amesisitiza kuwa pamoja na kusaidia jamii benki hiyo imeenda mbali zaidi, badala ya kutoa misaada mbalimbali pia wanayo akaunti maalum kwa ajili ya mashirika na taasisi za kijamii yaani ‘Organizations and Institutions with Social Impact’ inayoitwa “Community Account” ambayo haina malipo ya mwezi ya uendeshaji (no ledger fee) ambapo ameitaka Hospitali ya Mwananyamala kufungua akaunti hiyo kwa ajili kuendesha miradi yake.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyalama Dr. Sophinias Ngonyani akitoa shukrani kwa Benki ya KCB ambapo amesema vifaa hivyo vitasaidia kuokoa maisha ya watu na vimetolewa kwa wakati muafaka ambapo Hospitali hiyo ilikuwa ikivihitaji. Kulia ni Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye akikabidhi rasmi sehemu ya vifaa hivyo kwa Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyalama Dr. Sophinias Ngonyani. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Fedha ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Bw. Gofrey Ndalahwa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyalama Dr. Sophinias Ngonyani akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) namna ya kifaa hicho kinavyotumika. Katikati ni Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye na kulia ni Mkuu wa Fedha ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Bw. Gofrey Ndalahwa.
Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mwananyalama Dr. Sophinias Ngonyani akitoa mkono wa shukrani kwa Mkuu wa Fedha ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya KCB Tanzania Bw. Gofrey Ndalahwa (kulia). Wa pili kushoto ni Msimamizi wa Bima ya Afya katika Hospitali ya Mwananyamala Dr. Merina Nkullua na Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye.
Pichani ni baadhi ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Benki ya KCB wakati wa hafla fupi ya makabidhiano hayo kwenye makao makuu ya Ofisi za Benki hiyo Harambee Plaza jijini Dar.
Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa KCB Benki Bi. Christina Manyenye akisaidiana na uongozi wa Hospitali ya Mwananyamala kufunga vifaa hivyo.