Msanii aliyewahi kuwa mwimbaji wa Bendi ya African Stars International ‘Twanga Pepeta’, Khamis Kayumbu ‘a.k.a Amigolas (pichani) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu
MOblog inajaribu kufanya mawasiliano ya karibu kwa njia ya simu na mjomba wa marehemu Bw. Rajab Ahmed ili kujua marehemu alikuwa akisumbuliwa na maradhi gani.
MOblog inaunga na familia ya marehemu katika kuombeleza kifo cha Khamis Kayumbu na mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.
INNA LILAH WAINNA IRYH RAJIUN.