Anthony Banbury akiwa kwenye kikao maalum na Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf kwenye Ikulu ya nchini hiyo.
Na Mwandishi wetu
Afisa wa Umoja wa Mataifa anayehusika na mapambano dhidi ya maradhi ya Ebola ameionya jumuiya ya kimataifa isilegeze kamba katika harakati za kuyatokomeza maradhi hayo hatari
Akizungumza baada ya kukutana na rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf mjni Monrovia Afisa huyo Anthony Banbury amesema ingawa zipo dalili za kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo kila mtu anapaswa kuendelea kuwa makini
Banburry amesema umoja wa mataifa umejenga vituo vya kupambana na Ebola huku watu wa kujitolea wakiitajika kuviendesha vituo hivyo.
Wakati huo huo, shirika la afya ulimwenguni WHO limesema majaribio ya chanjo dhidi ya Ebola yameonyesha matumaini ya mafanikio.