Mkurugenzi Mtendaji wa Benki Mkombozi Commercial, Edwina Lupembe.
Na Mwandishi wetu
Benki ya Mkombozi nchini imesema kuwa mchango wa kifedha wanazopata katika shughuli za kijamii umekuwa wakimafanikio makubwa hasa kupitia uwekezaji wa sekta ya elimu Nchini, kwani hali hiyo inachangia kwa kasi maendeleo ya Taifa kwa kuwa na wataalamu wa Nyanja mbalimbali wenye uwezo mkubwa.
Taasisi za kifeda kama mabenki wamekuwa ni wadau wakubwa wa mchango huo, hivi karibuni benki ya mkombozi Tanzania inayomilikiwa na baraza la Maaskofu Tanzania (TEC)imejikita katika kuisaidia jamii kielmu kupitia kuwasaidia watoto yatima kwa kuwawezesha kielimu kupitia kugharamikia masomo yao.
Kituo cha watoto yatima cha kijiji cha matumaini(Village of Hope), kata ta Mkolani, Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza, kwa kuwasaidia watoto wao kuwasomesha masomo ya Sekondari hadi kidato cha sita (6).
Akiongea mbele ya vyombo vya habari meneja wa benki ya Mkombozi Jijini Mwanza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo bwana Nichorus , Nicholas Mokirya alisema kuwa wamekuwa na utaratibu wa kurudisha faida wanayoipata kwa jamii kupitia uwekezaji katika Nyanja ya kielimu.
Bwana Nichorus aliongeza kuwa wameamua kuwasaidia watoto watatu toka kituo hicho cha watoto yataima ambao ni Nancy Oscar mwanafunzi wa kidato cha tatu, wa pili ni Kashuliza Kamugisha kidato cha pili, na wa mwisho ni Peter Aklan anasoma kidato cha kwanza .wanafunzi hawa wanasoma shule ya sekondari ya Twihulumile iliyopo kata ya Butimba wilaya ya nyamagana wanaishi katika kituo cha kijiji cha matumaini nyegezi Mwanza .
Watoto hao wote watatu wamekuwa wakifanya vyema katika masomo yao hali ilioyowavutia benki ya Mkombozi kutoa msaada wa kielimu kuwasomesha wanafunzi hao hadi kiwango cha kidato cha sita.
“Tuna amini kuwa jamii yoyote ile ili iweze kuendelea lazima iwekeze kwenye elimu, hivyo basi sisi tumeamua kuwekeza kwa watanzania kwa kuwapa msaada kielimu kwani tuna amini kuwa jambo hili litakuwa la faida kwa jamii nzima na wala hatutajuta kwa uamuzi wetu huo, tunachokiomba ni juhudi zao watoto wote wanaowezeshwa na benki yetu katika kupata elimu ili waweze kutimiza ndoto zao”.
Jambo hilo lililofanywa na benki hiyo ni la mzingi sana kwani hata sera ya elimu ya mwaka 1995 inasisitiza kuwaendeleza wanafunzi na kuwatayarisha kikamilifu katika ngazi ya sekondari ili waweze kuja kuwa wataalumu wenye ujuzi katika ngazi za vyuo vya ufundi na vyuo vikuu.
Benki ya biashara ya mkombozi ilianza rasmi 28 Agosti 28, 2009 ikiwa na matawi manne matatu yako Dare es salaam na moja liko katika mkoa wa Mwanza, ambayo yanatoa huduma zote za kibenki na kuchochea maendeleo katika mfumo wa sayansi na teknolojia.
Kwa kuona umuhimu wa kuisadia jamii, benki hiyo iliweza kuisadia jamii iliyokumbwa na uyatima kwa kuwasomesha watoto watatu mwaka 2013 kutoka Jijini Dar es Salamu kwa kuwagaharamikia masomo yao sanjali na mwaka 2014 ilipoendeleza sera yake kwa kuwasaidia watoto wengine watatu toka Jijini Mwanza.
“Kwa upoande wangu mimi nawashukuru sana benki ya Mkombozi kwa kutusaidia, kwani naona sasa ndoto zangu za kuja kuwa Daktari zinatimia hasa leo nilipopata ufadhili huu wa masomo yangu, kwani sina ndugu wenye uwezo wa kunisaidia”. Alisema mwanafunzi Nancy Oscar wa kidato cha tatu anayesoma shule ya Sekondari ya Twihurumile kata ya Butima, Wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza mchepuo za sayansi.
Naye mwanafunzi mwingine Peter Aklani anayesoma kidato cha kwanza, mwenye ndoto z akuja kuwa injinia aliishukuru sana benki hiyo kwa kumsaidia na kuiomba iendelee kutoa elimu zaidi kwa watoto wengine yatima wasio kuwa na msaada ili waweze kukamlisha ndoto zao.
Ni wazi kuwa wewe msomaji wa makala hii unakumbuka kuwa Nchi yetu ya Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kila mtanzania anapata elimu bora kupitia mipango na mikakati mbalimbali ikiwemo ile ya malengo ya milleninia yanayotekelezwa na mpango wa MKUKUTA ili kufika mwaka 2015 basi Tanznaia iwe imepiga hatua kubwa ya maendeleo.
Kilichofanywa na benki ya Mkombozi ni mfano wa kuigwa kwa taasisi nyingine za kifedha hapa Nchini, kwani uwekezaji wa kilelimu ndiyo uwekezaji nambari moja kwa Nchi iliyo makini inayotaka kuendelea, ni mifano mingi tu inayotukumbusha mbali mfano wa zile Nchi za bara la Asia, ambapo miaka ya 1970 na 1980 tulikuwa katika mstari mmoja wa maendeleo lakini leo hii wenzetu wametuacha mbali sana, kwa kuwa walithubutu kuwekeza katika Nyanja ya elimu. Ongereni sana Mkombozi kwa kutumia jicho la tatu kuona mbali na kuamua kuipa kipaumbele cha kwanza elimu hasa kwa watoto wetu mayatima, huo ni mfano wa kuigwa.