Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta akizungumza katika sherehe za kuzindua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora, Margareth Sitta akizungumza katika sherehe za kuzindua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta, watatu kulia ni Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwansa.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Mbunge wa Urambo Mashariki, ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta (mwenye miwani ya jua nyuma ya Waziri Mkuu) wakikagua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katiak hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi kutoka kwa Wabunge Samuel Sitta na mkewe Margareth baada ya kuzindua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katiak hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Urambo, msaada wa vyandarua 100 na blanketi 300 kutoka kwa Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta katika mkutano wa hadhara aliohutubia mjini Urambo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika mkutano wa hadhara aliouhutubia mjini Urambo Oktoba 12, 2014. Kulia ni Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta na kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa..
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwaaga wananchi wa Urambo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa akizungumza katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Uyui Tabora.
Mbuge wa Igalula , Athumani Mfutakamba akizungumza katika Mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Uyui Tabora.