Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Mwanasheria wa Zanzibar afukuzwa kazi

$
0
0

omo

Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mhe. Pandu Ameir Kificho, (Kulia) na Mwanasheria Mkuu wa nchi ya Zanzibar, Othman Masoud Othman (mwenye suti ya kijivu), wakitokea mlango  wa nyuma wa jengo la bunge hivi karibuni, baada ya kutishiwa kupigwa na wajumbe wa bunge hilo la katiba kutoka nchini Zanzibar. Mhe. Masoud alipigia kura ya HAPANA rasimu inayopendekezwa kuwa katiba mpya ya nchi mbili Tanganyika.

Na Mwandishi wetu

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein amemtimua kazi Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar (AG), Othman Masoud Othman.

Hatua hiyo ya Dk Shein imekuja ikiwa ni wiki moja tangu mwanasheria huyo kukataa ibara 22 za Katiba inayopendekezwa wakati wa Bunge Maalum la Katiba, mjini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Dk Abdulhamid Yahya Mzee imesema Rais Shein amempandisha cheo aliyekuwa Naibu Mwanasheria Mkuu, Said Hassan Said kuwa AG.

“Amefanya mabadiliko hayo kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 kupitia Ibara ya 55(1), 53, 54(1) na 55(3)… Rais Shein ametumia Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2011, Kifungu cha 12(3) na 27,” ilisema taarifa hiyo.

Othman ambaye hivi karibuni alijiondoa katika Kamati ya Uandishi ya lililokuwa Bunge Maalumu kwa kutoridhika na baadhi ya mambo, alieleza bungeni kutokubaliana na ibara ya pili, tisa, 86, 37, 70 hadi 75 na Sura ya 11 ambayo ina ibara ya 158 hadi 161, Sura ya 16 yenye ibara za 243 hadi 251 na Nyongeza ya Kwanza inayozungumzia mambo ya Muungano.

Hatua hiyo ilionekana kuwaudhi baadhi ya wajumbe ambao walimzomea na baada ya Bunge kuahirishwa, alitolewa kupitia mlango wa nyuma wa Ukumbi wa Bunge chini ya ulinzi mkali.

Mwanasheria huyo alinukuliwa akisema alitumia utashi wake wa kidemokrasia kupiga kura kuzikataa ibara hizo, kutokana na kutoridhishwa na jinsi zilivyoandikwa.

“Katika suala la Katiba, Serikali ilishatamka kwenye Baraza la Wawakilishi na hata nje ya Baraza kwamba haina msimamo. Ndiyo maana uliona misimamo ilikuwa imeachwa kwenye vyama vya siasa, mimi siyo Mwanasheria Mkuu wa chama chochote.

“Kwa hiyo kama Serikali haikuwa na msimamo kwa maana ya upande… nilipiga kura kwa kuzingatia utashi wangu na maoni yangu.”


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles