Quantcast
Channel: Uncategorized – DEWJIBLOG
Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Brela yatoa siku 90 kwa makampuni

$
0
0

brela-june20-2014(1)

Na Mwandishi wetu

WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) umetoa siku 90 kwa wamiliki na wakurugenzi wa makampuni kuwasilisha taarifa zao za mwaka za mahesabu zilizokaguliwa na Mhasibu anayetambuliwa kisheria,  vinginevyo kampuni zao zitafutwa na wao kuchukuliwa hatua za kisheria.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa wakala huo na Msajili wa Makampuni, Frank Kanyusi, aliwaambia waandishi wa habari jiji Dar es Salaam jana kuwa wamiliki na wakurugenzi hao wa makampuni wanatakiwa kutumia siku hizo kuwasilisha taarifa zao za mwaka pamoja na  mahesabu ya kampuni, ili wasiweze kukabiliwa na sheria.

“Agizo hili la siku 90 sawa na miezi mitatu linaanza Oktoba 6, mwaka huu na litafikia kikomo Januari 5, mwakani ,”alisema.

Alisema kampuni itakayoshindwa kutekeleza agizo hilo ndani ya kipindi hicho itafutiwa usajili na wamiliki na wakurugenzi wake watafikishwa mahakamani kwa kosa la kutotoa taarifa za kampuni zao kwa mujibu wa sheria ya makampuni.

Aidha, matawi ya makampuni ya kigeni yaliyoandikishwa Tanzania pia yanapaswa kuwasilisha mahesabu ya kila mwaka, chini ya kifungu namba 438 kifungu kidogo cha kwanza cha sheria hiyo.

Alifafanua kwamba Tanzania ina kampuni 120,000 ambazo zimesajiliwa kisheria lakini ni kampuni 20,000 tu ndizo zinazotimiza wajibu wake wa kuwasilisha taarifa zake za kila mwaka.

 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 5755

Trending Articles