Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitazama ngoma ya Kihaya kabla ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba Oktoba 5, 2014 ambako alikuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za siku ya walimu duniani zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Oktoba 5, 2014. Wengine kutoka kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi na mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama, Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Mbunge wa Luangwa, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu, Fabiana Massawe.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na Mbunge wa Bukoba mjini, Hamisi Kagasheki kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba kabla ya kuondoka kuelekea Dodoma Oktoba 5, 2014. Mheshimiwa Pinda alikwenda Bukoba kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika sherehe za siku ya Walimu Duniani zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Kaitaba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na baadhi ya viongozi wa chama cha Walimu Tanzania kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba baada ya kuhutubia katika sherehe za siku ya walimu duniani zilizofanyika kitaifa kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba Oktoba 5, 2014.